HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA YAADHIMISHA SIKU YA UKIMWI DUNIANI, DC MBONEKO AKEMEA WIZI WA DAWA

 

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi duniani katika kijiji cha Ihalo Kata ya Ilola halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Na Marco Maduhu  -Shinyanga. 

Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, imeadhimisha siku ya Ukimwi duniani katika kijiji cha Ihalo Kata ya Ilola wilayani humo leo Ijumaa Novemba 27,2020.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, na kuhudhuriwa pia na watendaji wa halmashauri wakiongozwa na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Hoja Mahiba, ambapo kilele cha maadhimisho hayo ni Desemba Mosi mwaka huu. 

Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mboneko amewataka wananchi wasiwanyanyapae watu ambao wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, bali washirikiane nao katika shughuli mbalimbali za maendeleo. 

Amesema ugonjwa huo ni kama ugonjwa mwingine, hivyo siyo vyema kuwatenga watu wenye maambuzi ya virusi vya Ukimwi na kuwataka wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao mara kwa mara ili kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi. 

"Naombeni sana wananchi tuishi vyema na watu ambao wana maambukizi ya virusi vya Ukimwi, tusiwanyanyapae, na pia mpime afya zenu na kujikinga na maambukizi mapya," amesema Mboneko. 

"Pia watu ambao mnaendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU muendelee kutumia lakini pia wataalamu muwapatie huduma stahiki na kwa wakati," ameongeza. 

Katika hatua nyingine Mboneko, amekemea wizi wa madawa katika vituo vya kutolea huduma za afya, na kubainisha kuwa Serikali imekuwa ikisambaza dawa za kutosha, lakini anashangaa kusikia taarifa za uhaba wa dawa kuwepo kwenye baadhi ya hospitali. 

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Damas Nyansira, akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya Ukimwi wilayani humo, alisema kiwango cha maambukizi ni asilimia 3. 

Amesema katika halmashauri hiyo kuna jumla ya watu 74,862 wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, na wamesha unganishwa na huduma ya tiba na matunzo, na kubainisha kuwa changamoto zinazowakabili ni vituo vichache vinavyotoa huduma za CTC, ambapo vipo 10 na mahitaji ni 20. 

Amebainisha changamoto nyingine ni ushiriki duni wa jamii na hasa wanaume katika suala la upimaji VVU, ufinyu wa bajeti ya fedha kwa wadau wa UKIMWI na Serikali, kwa ajili ya kuendesha shughuli mbalimbali za UKIMWI katika Halmashauri, pamoja na upungufu wa dawa za kufubaza makali ya VVU kwa watoto. 

Nao baadhi ya watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi waliwataka wananchi kujenga tabia ya kupimwa afya zao na kuachana na mila potofu za kurogwa, ili kujitambua na kulinda afya zao, na watakaogundulika kuwa na maambukizi watumie dawa za kufubaza makali ili waishi miaka mingi. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya ukimwi katika kijiji cha Ihalo Kata ya Ilola wilayani Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiwataka wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao mara kwa mara, pamoja na kujiunga na mfuko wa bima ya afya CHF iliyoboreshwa. Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya ukimwi. Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Damas Nyansira akisoma taarifa ya hali ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi wilayani humo.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya Siku ya Ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi yakiendelea.
Maadhimisho ya siku ya Ukimwi yakiendelea.
Awali mkuu wa wilaya akikagua mabanda ya wajasiriamali, kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya akiendelea na zoezi la kukagua mabanda ya wajasiriamali, kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akipima uzito kwenye maadhimisho ya siku ya Ukimwi, wilayani Shinyanga.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Hoja Mahiba, akipima afya kwenye maadhimisho  ya siku ya Ukimwi.
Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Deus Muhoja, akipima afya kwenye madhimisho hayo ya siku ya Ukimwi.
Mwandishi wa habari wa ITV Mkoani Shinyanga Frank Mshana, akipima afya kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizindua zoezi la utoaji dawa za minyoo pamoja na vitamini A kwa watoto wenye kuanzia miezi Sita hadi Miaka Mitano, kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi.
Zoezi likiendelea.
Awali mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, kulia akiingia kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi, akiambatana na Jeshi la Jadi Sungusungu, kushoto ni Diwani mteule wa Kata ya Ilola Amos Mshandete.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye maadhimisho hayo ya siku ya Ukimwi.

Na Marco Maduhu- Shinyanga. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post