Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw.Biswalo Mganga akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi nchini kuacha kuficha Vifaa hivyo.
**
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Bw. Biswalo Mganga amewaonya wauzaji wa vifaa vya Ujenzi kufuatia baadhi yao kuficha Simenti na Mabati kwa lengo la kuongeza bei ili kujipatia faida kubwa zaidi, na kusema kuwa kufanya hivyo ni kosa la Jinai.
Bw. Mganga ameeleza kuwa watu wote wanaofanya hivyo wanafanya kosa la uhujumu uchumi ambalo limeanishwa katika Sheria ya Uhujumu Uchumi ambapo adhabu yake ni kifungo cha miaka 20 jela pamoja na kutaifishwa mali kwa yeyote atakayekamatwa kwa kutenda kosa hilo.
Mkurugenzi wa Mashtaka amebainisha hayo Jijini Dodoma leo wakati wa mahojiano maalum yaliyofanyika yaliyokuwa na lengo la kufahamu mafanikio ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka tangu kuanzishwa kwake ambapo ameeleza kuwa imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake.
Aidha, amesema kuwa jukumu la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka ni kuhakikisha kuwa Haki, Amani na Usalama vinapatikana nchini kwa Maendeleo ya Taifa. Mwonekano wa nembo ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma
Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini Biswalo Mganga akusoma Dira ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka
Mwonekano wa mbele wa jengo la Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS) lililoko Jijini Dodoma