Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Matiko kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Esther Bulaya kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai akimwapisha mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Cecilia Pareso kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA Mheshimiwa Halima Mdee akiongea jambo kwa niaba ya Wabunge wengine wa CHADEMA walioapishwa hii leo kwenye Viwanja vya Bunge Jijini Dodoma.
Wabunge Wateule wa Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo – wakisubiri kula kiapo kwenye viwanja vya Bunge Jijini Dodoma leo.
***
Wabunge wateule wa viti maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Halima Mdee, wamekula kiapo hii leo katika viwanja wa Bunge jijini Dodoma.
Zoezi la uapisho wa wabunge hao limeongozwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, leo Novemba 24, 2020.
Akizungumza mara baada ya kula kiapo, Halima Mdee amesema kuwa, "Nakishukuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, ambao kupitia wao sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu, viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata".
Wabunge hao walioapishwa ni pamoja na Halima Mdee, Grace Tendega, Ester Matiko, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnester Kaizer, Nusra Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga na Tunza Malapo.
Wengine ni Asia Mohamed, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majela,Stella Fihaya, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchester Lwamlaza.