MBUNGE
wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania
Bara Neema Lugangira akila kiapo cha kuwa mbunge Bungeni |
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira kushoto akila kiapo cha kuwa mbunge Bungeni |
MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania Bara Neema Lugangira waliosimama nyuma wa nne kutoka kushoto akiwa kwenye picha ya Pamoja na Rais Dkt John Magufuli aliyekaa katikati kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu na kulia ni Spika wa Bunge Job Ndugai ,Waziri Mkuu Kasim Majaliwa na kwanza kushoto ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Hasani Mwinyi
NA MWANDISHI WETU, DODOMA.
MBUNGE
wa Viti Maalumu kupitia kundi la Asasi za Kiraia nchini (NGOs) Tanzania
Bara Neema Lugangira amesema hotuba ya Mhe Rais Dkt John Magufuli
imemgusa baada ya kuona namna alivyogusia makundi yake ya kipaumbele cha
kwanza uwezeshwaji kiuchumi wanawake na mikopo isiyokuwa na riba na
yenye riba unafuu.
Neema
aliyasema hayo ikiwa ni muda mchache mara baada ya Hotuba hiyo ya Mhe
Rais Dkt John Magufuli wakati akilifungua Bunge la 12 jijini Dodoma
ambapo alisema pia imewagusa wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na
wazee.
Alisema pia
aligusia kwa mapana mambo ambayo serikali yake kwa kipindi cha muhula
wake wa pili itakayokwenda kuifanya kwa ajili ya wazee hali iliyompa
faraja kuona nafasi yake binafasi tayari kwa kuchangia kikamilifu kwenye
utekelezaji wa Ilani ya CCM na dira ambayo Rais amewapatia.
“Lakini
pia nimeguswa na mpango mkakati wa serikali kwenda kuboresha mazingira
wezeshi ya biashara kwa nia ya kuongeza uwekezaji ambao utapelekea
kuongeza ajira na kuinua uchumi kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa
ujumla”Alisema
Aidha
alisema kwamba hotuba hiyo imemfariji maana amegusa kwa ukamilifu sekta
ya kilimo na umuhimu wa kuunganisha sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi na
sekta binafsi.
“Kama
unavyofahama masuala mengi yanayofanywa ngazi ya jamii yanafanywa na
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na asasi za kiraia hivyo mimi kama
mwakilishi wa NGOs Bungeni kitu cha kwanza ni kuanza kuzitambua NGOs
kwenye maeneo hayo ya kipaumbele ambayo Mhe Rais amewaambia leo
yanafanya nini” Alisema
Mbunge
huyo alisema pia ataweka kipaumbele kikubwa kuelewa wafadhili wa NGOs
hapa Tanzania na wadau wa maendeleo wanafadhili kwenye maeneo gani kisha
waone hayo maeneo wanayofadhili kama yanaenda sambamba na dira ya
serikali na dira ya Mhe Rais.
“Lakini
kama hayaendani sambamba nini kifanyike kwahiyo mimi nitakuwa kiungo
kati ya mashirika yasikuwa ya kiserikali, bunge na serikali pamoja na
wafadhili” Alisema