Spika wa Bunge anayemaliza muda wake, Job Ndugai amechukua fomu kwa ajili ya kutetea nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
Ndugai ambaye amekuwa katika nafasi hiyo katika Bunge la kumi na moja amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo na kuirejesha leo katika ofisi makao makuu ya CCM jijini hapa.
Akizungumza baada ya kurejesha fomu kwa Katibu msaidizi idara ya oganaizesheni CCM Taifa, Solomon Itunda, Ndugai amewaomba Watanzania wamuombee ili chama kimteue katika nafasi hiyo.
"Ni utaratibu wa chama chetu wa kidemokrasia kuruhusu wanachama wenye sifa kugombea nafasi ya Spika na Naibu Spika kisha kufanya uteuzi. Niwaombe Watanzania waniombee ili niteuliwe na niwaambie kuwa wakati ukifika tutaongea nao," amesema Ndugai.
Social Plugin