Mwanamke mmoja kaunti ya Kiambu nchini Kenya ameripotiwa kumkata mwanawe wa umri wa mwaka mmoja na miezi 8 sehemu nyeti kisha kuzitupa chooni.
Haijabainika ni kwa nini mama huyo alitekeleza kitendo hicho ila maafisa wa polisi wameanza kufanya uchunguzi kufuatia kisa hicho.
Babake mtoto huyo aliripoti katika kituo cha polisi cha Tigoni akidai kuwa Winnie Mutheu ambaye alikuwa mkewe alitoroka baada ya kutekeleza kitendo hicho.
Kulingana na jirani, mwanamke huyo alitupa sehemu za siri za mwanawe kwenye choo kabla ya kutorokea mafichoni.
Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Tigoni Mwaniki Irei alisema mtoto huyo amelazwa katika hospitali ya Kijabe akiwa hali mahututi.
Afisa anayeshughulika maslahi ya watoto eneo la Tigoni George Ngugi amesema watashikiriana na maafisa wa polisi kuhakikisha mshukiwa anakamatwa na kukabiliwa vilivyo kisheria.
Visa vya aina hii vimekithiri nchini, mapema wiki jana mama mmoja kaunti ya Nakuru alimuua mtoto wake wa miaka mitatu baada ya kugombana na mumewe.
Kulingana na taarifa ya polisi, mshukiwa Faith Chepkemoi Maritim alitekeleza kitendo hicho kufuatia mzozo wa kinyumbani wa mara kwa mara kati ya na mumewe Benard Maritim.
Chepkemoi aliambia polisi kwamba alikuwa amechoshwa na ndoa hiyo na ndiyo sababu aliamua kujinyakulia mpenzi mpya ambaye tayari alikuwa ameahidi kumuoa.
Via>>Tuko News
Social Plugin