Baraza la Mawaziri wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama wamekutana katika mkutano wa dharura na kujadili masuala ya siasa, ulinzi na usalama.
Mkutano huo umefanyika mjini Gaborone, Botswana ambapo ulitanguliwa na mkutano wa Makatibu Wakuu wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama ulioanza asubuhi na kumalizika mchana.
Kupitia mkutano huo, mawaziri wameweza kujadili masuala ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC na kupendekeza njia mbalimbali za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza kwenye siasa, ulinzi na usalama ndani ya ukanda wa SADC.
Pamoja na mambo mengine, Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama inawajibika kukuza amani na usalama katika eneo la SADC na pia ina wajibu wa kuongoza na kuzipatia nchi Wanachama mwongozo kuhusu mambo ambayo yanatishia amani, ulinzi na usalama.
Social Plugin