MBUNGE MTEULE PEKEE CHADEMA ASEMA ATAENDA BUNGENI KUAPISHWA..."SITOWASALITI WANANCHI WALIONICHAGUA"
Tuesday, November 03, 2020
Aida Khenan, Mbunge Mteule wa Nkasi Kaskazini kupitia CHADEMA amesema, hatowasaliti wananchi waliomchagua hivyo atakwenda Bungeni kuapishwa ili aweze kuwatumikia.
Aida ni Mgombea pekee wa Ubunge kupitia CHADEMA aliyetangazwa mshindi katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, akimshinda Ally Kessy wa CCM aliyekuwa anatetea jimbo hilo aliloongoza kwa miaka 10.
Kauli hiyo imekuja baada CHADEMA na ACT-Wazalendo kutangaza kutoyatambua matokeo ya Uchaguzi yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) hata kwenye maeneo waliyoshinda.
Katika Bunge lililopita, Aida alikuwa Mbunge wa Viti Maalum. Lakini sasa amesema yeye ni Mbunge ambaye anasubiri kuapishwa.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin