Mkurugenzi wa Rasilimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi Mary Mwangisa, akitoa maelekezo wa baadhi ya watalaam watakaoshiriki katika elimu ya mafunzo na matunzo ya miondombinu ya umwagiliaji kwa wakulima.Mkurugenzi msaidizi wa idara ya mafunzo na matunzo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Enterbert Nyoni akifafanua jambo wakati wa kikao na wataalam,cha maandalizi ya utoaji elimu kwa wakulima kuhusiana na utunzaji wa miundominu ya Umwagiliaji.kulia, ni Bw.Reginald Diamett Meneja Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiliaji.
Picha ikionesha sehemu ya washiriki katika kikao hicho cha maandalizi.
Na MwandishiWetu Dodoma
Mkurugenzi
Rasimali watu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bi. Mary Mwangisa,
amewapa maekelezo baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo watakaoshiriki
katika zoezi la utoaji elimu na mafunzo ya utunzaji wa miundombinu ya
kilimo cha umwagiliji katika baadhi ya skimu za kilimo hicho nchini.
Akikaimu
nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo, Bi Mwangisa amesema kuwa
watumishi hao wanapaswa kuzingatia mwongozo wa namna ya kutoa mafunzo ya
vyama vya umwagiliaji wa namna ya kukusanya mapato kwa ajili ya
uchangiaji wa mfuko wa maendeleo ya umwagiliaji, matumizi sahihi ya
kalenda za kilimo na utunzaji wa miundombinu ya umwagiaji.
“Serikali
imewekeza pesa nyingi katika miundombinu ya umwagiliaji kwa hiyo
isipotunzwa serikali itapata hasara, na wakulima wataathirika, vyama vya
umwagiliaji vitakufa na miundombinu hiyo itakufa.” Alisisitiza.
Aliendelea
kusema kuwa kilimo cha umwagiliaji ni moja kati ya mategemeo ya
kuongeza uzalishajiwa mazao ya chakula na biashara na uhakika wa usalama
wa chakula nchini.
Maelekezo hayo kwa watumishi yametolewa ikiwa
ni sehemu ya maandalizi ya mkakati wa tume ya taifa ya umwagiliajiwa
kutoa elimu kwa vyama vya umwagiliaji nchini.