MUUGUZI, DAKTARI MBARONI KWA WIZI WA MASHINE ZA MIL. 26 CHUMBA CHA UPASUAJI HOSPITALI YA RUFAA SHINYANGA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linamshikilia Mtumishi wa Idara ya Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga Madaraka Joseph (32) na Mmiliki wa Zahanati ya Suka ( Suka Wazazi Dispensary) , Dk. Suka Charles kwa tuhuma ya wizi wa vifaa tiba zikiwemo mashine za kuangalia wagonjwa zenye thamani ya shilingi milioni 26 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. 

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo,Jumamosi Novemba 7,2020, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema wizi huo umetokea Oktoba 13,2020 majira ya saa 10 jioni katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 

Kamanda Magiligimba amesema Oktoba 13,2020 kulitokea wizi wa mashine mbili za kuangalia wagonjwa katika chumba cha upasuaji aina ya EDAN 1M8 na DATA SCOP 1 zenye thamani ya shilingi milioni 26 mali ya Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. 

“Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga likaanza uchunguzi wake mara moja na kubaini kuwa mtuhumiwa Madaraka Joseph, Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga na mkazi wa Mageuzi Mjini Shinyanga ambaye ni Mtumishi wa Idara ya Chumba cha Upasuaji ndiye aliyeziiba mashine hizo na kwenda Kuuza kwa Dk. Suka Charles ambaye ni Mmiliki wa Suka Dispensary iliyopo wilayani Kahama ambaye ni mkazi wa Buzuka Mjini Shinyanga na makazi mengine wilayani Kahama”,ameeleza Kamanda Magiligimba. 

“Muuguzi huyo wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Madaraka Joseph aliuza mashine hizo kwa Suka Charles kwa makubaliano ya Shilingi Milioni 4 ambapo alishatanguliziwa shilingi milioni 2”,amesema Kamanda Magiligimba. 

Kamanda huyo wa polisi amesema baadae Suka Charles alikamatwa na upekuzi ulifanyika nyumbani kwake maeneo ya Mhongolo wilayani Kahama na kufanikiwa kupata mashine hizo (EDAN 1M8 na DATA SCOP 1) zikiwa na vifaa vyake. 

Amevitaja vifaa hivyo kuwa ni Patient Monitor mbili, BP mashine accessories 5,cable wires accessories 7,medical molecular sieve,Oxygen Concentrator na Oxygen Concentrator Intesty. 

Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika. 

Ametoa wito kwa watumishi kuacha tabia ya wizi wa mali za umma zinazotokana na tama ya mafanikio ya muda mfupi ambapo hupelekea wananchi kukosa huduma hivyo kuibebesha lawama serikali. 

Hata hivyo amesema Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga litaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote au watumishi wa serikali watakaobanika kufanya uhalifu wa aina yoyote ile.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akitoa taarifa kwa vyombo vya habari leo Jumamosi Novemba 7,2020 kuhusu wizi wa vifaa tiba uliotokea Oktoba 13,2020 majira ya saa 10 jioni katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba akionesha sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 26 vilivyoibiwa katika Chumba cha Upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post