Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo Novemba 13, 2020, wakati akihutubia na kufungua bunge la 12, kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
“Nitashirikiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kulinda amani, hatutakuwa na utani hata kidogo na mtu atakayetaka kuvuruga amani na kuingilia uhuru wetu, na namuahidi Rais Dkt. Mwinyi nitampa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha aliyoyaahidi”, amesema.
Aidha Rais Magufuli amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuboresha mazingira kwa wananchi kuongeza kipato chao ikiwemo mazingira wezeshi ya biashara.
''Katika miaka mitano hii serikali ninayoiongoza itafungua milango ya majadiliano na sekta binafsi na wafanyabishara wote ili kujadili namna ya kuondoa migogoro ya biashara ili tutengeneza mabilionea wengi wakiwemo wabunge'', ameongeza.
Social Plugin