Dr Magufuli ameyasema hayo leo tarehe 13 Novemba, 2020, wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Bunge la 12 jijini Dodoma ambayo ilitoa dira ya uongozi wake katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Tutaanza kutenga fedha kidogo kidogo kwa ajili ya kuzianda timu zetu za Taifa na katika hilo napenda kutumia fursa hii, kuitakia heri timu yetu ya Taifa kwenye mechi yao dhidi ya Tunisia hapo baadaye,” alisema Magufuli.
Aidha Rais Magufuli aliongezea kwa kumtakia heri bondia Mtanzania Hassan Mwakinyo ambaye anashuka ulingoni hapo baadaye, kupambana na bondia kutoka nchini Argentina kwenye pambano la raundi 12 la ubingwa wa mabara wa IBF.
“Na pia nataka kumtakia heri mwanamasumbwi wetu, Hassan Mwakinyo anayepambana leo, watanzania tunataka ushindi tumechoka kushindwa,” aliongezea Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo Serikali itatenga kiasi kidogo cha fedha katika kuziandaa timu mbalimbali za Taifa na pia alitumia fursa hiyo kwa kuitakia heri Taifa Stars kwenye mchezo wake wa leo dhidi ya Tunisia.