Rais Magufuli amesema katika awamu yake ya kwanza madarakani alihakikisha nchi inakuwa na amani huku akivipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kulinda mipaka ya nchi.
Ameeleza hayo leo Ijumaa Novemba 13, 2020 bungeni mjini Dodoma katika hotuba yake ya kulizindua Bunge.
Amesema Watanzania wameendelea kuwa wamoja licha ya kutofautiana katika dini, kabila na itikadi ya vyama vya siasa.
“Wakati naingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la mauaji ya kutumia silaha mfano matukio ya Kibiti lakini kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na vyombo vya dola yalikomeshwa na kwa sasa nchi yetu ipo salama.
“Nchi yetu imeendelea kuwa kisiwa cha amani na mipaka yake imebaki kuwa salama. Navipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi kubwa waliyofanya ya kusimamia amani na niwashukuru pia Watanzania kwa kutoa ushirikiano kwa vyombo hivi.” Amesema
Social Plugin