Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akizungumza kwenye mafunzo namna ya uaandaji wa bajeti inayomhusu mtoto.
Shirika la Save The Children linalotetea haki za watoto, limetoa mafunzo ya mchakato wa bajeti inayomhusu mtoto ngazi ya halmashauri, ili kuisaidia Serikali uaandaji wa bajeti nzuri ambayo itatoa haki za watoto na kukidhi mahitaji yao.
Mafunzo hayo ambayo yalianza jana na yamekoma leo, yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Empire, yameshirikisha watendaji wa Kata, wataalamu kutoka halmashauri ya manispaa ya Shinyanga, waandishi wa habari, pamoja na wadau kutoka asasi za kiraia.
Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, amesema lengo la mafunzo hayo ambayo yamedumu kwa siku mbili, ni kuwajengea uwezo wadau mbalimbali katika kushiriki kikamilifu kuandaa masuala ya bajeti, na kutambua wajibu wao katika kushiriki uundaji wa bajeti.
Amesema katika mchakato mzima wa uaandaji wa bajeti za watoto, ni vyema bajeti hizo zikashirikisha watoto wenyewe katika utoaji wa mapendekezo yao ili kutambua nini wanakihitaji kutekelezewa, kuliko kuipitisha tu kwa mazoea na kuendelea kuwanyima haki zao za msingi.
“Save the Children tunataka upangaji wa bajeti za watoto zishirikishe watoto wenyewe katika utoaji wa mapendekezo, ili kujua nini wanakihitaji, mfano katika masuala ya ukatili ambayo tunakumbana nayo moja ya sababu ni umbali wa shule, hivyo katika upangaji wa bajeti ya watoto ukiwashilikisha huenda wakatoa maoni ya kutaka kujengewa shule karibu,” amesema Enock.
“Ukishirikisha watoto kwenye uaandaji wa bajeti yao, itatoa fursa kwa maendeleo ya mtoto bila ya ubaguzi, kutambua mahitaji maalumu ya watoto, pia kutambua mtiririko wa maamuzi katika matumizi ya rasilimali zinazolenga watoto,” ameongeza.
Naye mwezeshaji wa mada ya uaandaji wa bajeti, Afisa mipango Mwandamizi Ofisi ya Rais tawala za mikoa Zanzibar Masika Baraka, amesema uaandaji wa bajeti nzuri ni ile ambayo inashirikisha walengwa husika, katika utoaji wa mapendekezo ili kujua nini wanakihitaji.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo akiwamo mkurugenzi wa Shirika la Investing Childern and their Society mkoani Shinyanga (ICS) Kudely Sokoine, wameshukuru kupewa elimu hiyo, ambayo wamebainisha imewaongezea ufanisi katika utendaji wao kazi, hasa kwenye utekelezaji wa miradi ya watoto.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akizungumza kwenye mafunzo namna ya uaandaji wa bajeti inayomhusu mtoto.
Mratibu wa mradi wa mijadala jumuishi katika masuala ya uchumi na utawala wa kifedha Alex Enock kutoka Shirika la Save The Children mkoani Shinyanga, akizungumza kwenye mafunzo namna ya uaandaji wa bajeti inayomhusu mtoto.
Mwezeshaji wa mada ya uaandaji wa bajeti, Afisa mipango Mwandamizi Ofisi ya Rais tawala za mikoa Zanzibar Masika Baraka, akitoa elimu hiyo kwa washiriki.
Mwezeshaji wa mada kwenye mafunzo hayo mchumi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Allex Mpasa, akitoa elimu kwa washiriki.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo namna ya uaandaji wa bajeti inayomhusu mtoto.
Washiriki wakiwa kwenye mafunzo namna ya uaandaji wa bajeti inayomhusu mtoto.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
Washiriki wakiendelea na mafunzo.
John Shija kutoka Shirika la (PACESHI) Mkoani Shinyanga, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Kudely Sokoine kutoka Shirika la (ICS) Mkoani Shinyanga akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
John Eddy kutoka Shirika la (YWCA) akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Mwakilishi wa shirika la Women Fund Tanzania Mkoani Shinyanga Glory Mbia, akichangia mada kwenye mafunzo hayo.
Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mafunzo ya siku mbili yaliyojikita namna ya kuandaa bajeti inayokidhi mahitaji ya wananchi, wakiwamo watoto, yalioandaliwa na Shirika la Save The Children.
Na Marco Maduhu- Shinyanga.