AFISA wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga Gibson George akizungumza wakati wa mkutano huo
MKURUGENZI Mkazi wa Kampuni ya Simba Cement Mhandisi Benedict Lema akichangia jambo kwenye mkutano huo
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu wadau wa mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali
SEHEMU ya Wadau wa Viwanda mkoani Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali
NAIBU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) Latifa Mohamed Khamisi amesema kwamba watashirikiana kwa ukaribu na wenye viwanda mkoani Tanga kuhakikisha wanafanikiwa na kuendelea kukua kibiashara.
Latifa aliyasema hayo leo wakati wa mkutano wake na wadau wa viwanda Mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambapo wamefika mkoani Tanga kuona namna ya kutatua changamoto za wenye viwanda hatimaye viweze kuzalisha na kuuza kwenye masoko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma
Alisema hilo litasaidia kwa asilimia kubwa kurudisha enzi za miaka ya nyuma ambako kulikuwa na masoko mpaka ya ukanda wa afrika masharika pamoja na masoko ya ndani ili kuwawezesha kuweza kunufaika kupitia viwanda hivyo.
“Leo tumefika mkoani Tanga kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella tunatoa shukrani kwa kutupokea na kukubali agizo la Rais la Tanzania ya Viwanda”Alisema
Alisema kwamba mkoa huo unawaunga mkono kwenye maandalizi ya maonyesho makubwa ya kitaifa ya viwanda vya Tanzania kwa kushirikiana na mkoa kuhamasisha viwanda vya Tanga kuweza kushiriki.
“Kama unavyofahamu Tanga kulikuwa na historia kubwa ya viwanda ambavyo vilikuwa vinauza bidhaa kwenye ukanda wa Afrika vilikuwa vinatoka Tanga lengo la RC ni kuhakikisha viwanda hivyo vinafufuka na ndio maana tupo hapa kwa kushirikiana na mkoa tumefika kuhamasisha ushiriki wa maonyesho ya Tano ya viwanda vya Tanzania”Alisema
Alisema kwamba maonyesho hayo ni fursa adimu kwa viwanda ikiwemo kujifunza na kujua mashine na kuwakutanisha wazalishaji wa mali ghafi na wenye viwanda wenyewe kutatua changamoto za maendeleo ya viwanda.
Awali akizungumza katika mkutano huo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella alimshukuru Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade kwa kuandaa mkutano huo wa wamiliki na wazalishaji katika sekta ya viwanda kwenye mkoa wa Tanga.
Alisema kikao hicho ni mahususi kuona changamoto ambazo zinawakabili lakini kuona namna nzuri wanaweza kushiriki kwenye maonyesho ya Tan Trade yatakayoanza Desema 3-9 mwaka huu.
Alisema kwao ni fursa kwa wazalishaji na viwanda ikiwemo wakazi wa mkoa huo kwa sababu kadri viwanda vinavyozidi kupanuka kimasoko ndio uzalishaji unaongeza na unapoongeza unasaidia uhitaji wa malighafi na wafanyakazi ili uweze kuongeza uzalishaji.
“Niwashukuru Tan Trade kuendesha kikao hichi na kuamua kuja Tanga kwa sababu Tanga ni viwanda na viwanda ni Tanga lakini la la pili uwepo wa maonyesho hayo ni fursa kwa wawekezaji watatumia nafasi hiyo kujitangaza na kujifunza na kuona fursa zinazopatikana kwenye maonyesho”Alisema
Hata hivyo alisema wao kama mkoa watahakikisha Tantrade na wenye viwanda kuendelea kuwapa ushirikiano ili dhamira ya Rais ya yenzi wa uchumi wa viwanda iweze kufikiwa kwa kiwango kikubwa na kuwa na tija kubwa.