Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TIGO YATOA ZAWADI ZA SIMU JANJA ZAIDI YA 100 KWA WASHINDI WA MWANZO WA KAMPENI YA NCHI NZIMA YA ‘JAZA TUKUJAZE TENA’

 Dar es Salaam, Ijumaa, 6 Novemba 2020 – Kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania, leo imetoa zaidi ya simu janja 100 kwa washindi wa mwanzo wa kila siku na wiki wa kampeni ya ‘Jaza Tukujaze Tena’ inayoendelea nchi nzima.

Kampeni hiyo ambayo ilizinduliwa tarehe 23 Oktoba mwaka huu, itafanyika kwa kipindi cha miezi mitatu huku ikiwapa fursa wateja wa Tigo kuweza kujishindia zaidi ya simu janja 1200 pamoja na ofa za papo kwa papo kila wanaponununua vifurushi vya muda wa maongezi, SMs pamoja na data.

Simu janja zinazoshindaniwa ni pamoja na Samsung Note 20, ITEL T20 na Smart Kitochi. Simu zote hizi zinasubiri washindi ambao ni wateja wote wa Tigo, wauzaji wa jumla wa bidhaa za Tigo, Mawakala, Viongozi wa timu za mauzo, na watoa huduma wakubwa wa huduma za Tigo pesa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi simu janja kwa washindi, Meneja wa Tigo, kitengo cha Bidhaa, Suleiman Bushagama, amesema, “Tangu tuzindue kampeni hii, tumetoa zawadi ya dakika za muda wa maongezi zaidi ya milioni 149, MB za data milioni 504 na SMS milioni 81 kwa wateja wetu nchi nzima ambao walinunua vifurushi tangu kuzinduliwa kwa kampeni hii. Leo hii tunakabidhi simu janja kwa washindi wa kila siku na wiki”.

Ili wateja waweze kupokea ofa za papo hapo, wanapaswa kununua aina yoyote ya kifurushi, kiwe cha siku, wiki au mwezi kupitia njia zote za manunuzi zinazotambuliwa na Tigo ikiwa ni pamoja na kupitia menu kuu ambayo ni *147*00#, Tigo Pesa App na Tovuti. Baada ya manunuzi, wateja wataingizwa moja kwa moja kwenye droo ambayo itakuwa inawaweka kwenye nafasi nzuri ya kujishindia simu janja.

Wauzaji wa jumla wataingizwa kwenye droo hii moja kwa moja na watakuwa na nafasi ya kuibuka washindi wa simu janja endapo watauza aina yoyote ya kifurushi cha Tigo kupitia Tigo Rusha.

Frank Lyakurwa ambaye,ni mstaafu, kutoka Madale, Dar es Salaam, amejishindia simu janja ya Samsung Note 20 na amefurahi sana baada ya kuibuka mshindi. “Nilinunua bando la internet la wiki kwa shilingi 3,000 ambapo nilipewa bonus ya GB 2, baada ya hapo nilipigiwa simu kwamba nimejishindia Samsung Note 20. Sikuamini,” amesema.

“Nimefurahi sana,” amesema Jorum Mwakipesile kutoka Shinyaanga baada ya kujishindia simu janja ya Itel T20. “Kama ilivyo ada yangu, nilinunua bando la siku la shilingi 500 na kupata ofa ya dakika 10 za muda wa maongezi kwenda mitandao yote. Pia nilifahamishwa kwamba nimejishindia simu ya Itel T20, hii itanisaidia sana kusukuma mbele gurudumu la maisha,” amesema kwa furaha.

Tigo Tanzania inapenda kuwataadharisha wateja wake wote kwamba wawe makini na matapeli wanaoweza kuibuka kupitia mgongo wa kampeni hii. Wateja wanapaswa kufahamu kwamba, zawadi zote za bando zitakuwa zinatolewa papo hapo mara tu baada ya mteja kununua bando.

Pia washindi wa simu janja wa kila siku pamoja na wiki watapigiwa simu na mfanyakazi wa Tigo kupitia namba maalumu ya kampuni mara tu baada ya droo hizo kufanyika. Ofa hii ni bure, washindi hawapaswi kutoa malipo ya aina yoyote ili kupata zawadi zao. Wateja wote wa Tigo wanashiriki katika ofa hii.

https://www.youtube.com/watch?v=bC2kJhmCnE0&t=9s

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com