Kaimu MKurugrnzi Mkuu Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Daudi Kaali
akizungumza mapema leo kuhusu shughuli za Ofisi hiyo pamoja na ukarabati wa
Miundombinu ya Umwagiliaji unaoendela Mkoani Iringa. |
Bw. Reginald Diamett Meneja Mfuko wa Maendeleo ya kilimo cha umwagiliaji toka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, akiongea kuhusu shughuli za mfuko huo.
NA MWANDISHI WETU – DODOMA
Tume ya Taifa ya
umwagiliaji inaendelea na shughuli za maboresho ya miondombinu
inayopeleka maji katika skimu za kilimo cha umwagiliaji za Ruaha
Mbuyuni, Namagozi na Mlenge Pawaga MkoaniI ringa,iliyoharibiwa na
mafuriko katika msimu wa mvua zilizopita.
Hayo yameelezwa mapema
leo na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiaji Bw. Daudi
Kaali ambapo amesema katika skimu ya Ruaha Mbuyuni kazi ya kuchimba
nakupanga mawe katika njia mpya yenye urefu wa mita 600 inakaribia
kukamilika halikadhalika katika skimu za pawaga njia mpya yenye urefu wa
mita 800 inachimbwa.
“Asimia (60%) yaukarabati wa miundombinu
imekamilika katika skimu hizo, hivyo tunategemea mpaka mwishoni mwa wiki
hii kazi itakuwa imekwisha kabisa.” Alisema Kaali
Akizungumzia
Mradi wa Regrow unaosimamiwa na Wizara ya Maliasili na kutekelezwa na
sekta husika Bw. Kaali alisema kuwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ina
kazi ya kuimarisha miundombinu ya umwagiliaji ili kuweza kuleta ufanisi
mkubwa wa matumizi sahihi ya maji iliyaweze pia kutumika katika hifadhi
za taifa za ukanda wa kusini pamoja na shughuli nyingine za miradi ya
maendeleo.
“Tume ina jukumu la kujenga Mfereji mkubwa wa maji
wenye urefu wa kilometa tatu, kazi ambayo imefikia hatua yakutafuta
mkandarasi kwa ajili ya ujenzi huo katika skimu ya kilimo cha
umwagiliaji ya madibila na unategemea kuanza mwezi ujao.” Alifafanua.
Akizungumza
kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Kilimo cha Umwagiaji pamoja na mambo
mengine unasimamia pia shughuli za maboresho ya miundombinu ya kilimo
hicho.
Meneja wa Mfuko huo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw.
Reginald Diamett alisema lengo lingine la mfuko pia ni kujenga uelewa
kwa wakulima na kuhamasisha tozo na makusanyo ya ada za hudu ma za
umwagiliaji, jambo ambalo litaleta matarajio makubwa ya makusanyo katika
sekta ya Umwagiliaji.
“Matarajio ni kwamba katika hekta zaidi ya
laki sita zinazo mwagiliwa kwa sasa, katika msimu wa mavuno unaokuja,
zaidi ya shilingi Bilioni hamsini na mbili (Bilioni 52) zinaweza
kukusanywa ambapo Asilimia 75 (75%) itabakia kwa wakulima na asilimia
ishirini na tano (25%) ndiyo itakayochangiwa katika mfuko wa
umwagiliaji kama ada ya huduma ya umwagiliji.” Alibanisha.
Akizungumza
kuhusu ushiriki wa kada mbalimbali za watumishi wa Tume katika
kipengele cha kutoa elimu kwa wakulima Mkurugenzi wa Utawala na
Rasimaliwatu Bi. Mary Mwangisa amesema kuwa hili linachangia kuwajengea
uwezo wafanyakazi wa ndani kuhusu shughuli za Tume kuwa na uelewa pamoja
na kuboresha kada mbali mbali katika sekta ya umwagiliaji Jambo ambalo
pia limepelekea kupanua sekta hiyo kwa kuwapeleka watalam wa umwagiliaji
katika ngazi za mikoa na wilaya.
Kwalengo la kusogeza huduma ya umwagiliaji karibu zaidi na wakulima ambao wengi zaidi wapo katika maeneo ya vijijini.
Social Plugin