Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI MBALIMBALI DUNIANI WAENDELEA KUMPONGEZA JOE BIDEN KWA USHINDI


 Ushindi wa Joe Biden umepongezwa na viongozi mbalimbali duniani, wengi walieleza matumaini ya ushirikiano baina ya nchi baada ya miaka minne ya kuanguka kwa diplomasia chini ya Rais Donald Trump.

Wakati Trump akiendelea kupinga matokeo ya uchaguzi uliompa ushindi Biden, viongozi wengi duniani wameeleza wazi kuwa wanaunga mkono ushindi wa Biden na mgombea mwenza Kamala Harris.

Biden wa chama cha Democrats  amechaguliwa Rais wa 46 wa Marekani  baada ya kuhudumu kwa miaka 36 katika Baraza la Seneti la Marekani na miaka minane kama makamu wa Rais chini ya Rais wa zamani Barack Obama.

“Hongera! Nakutakia heri na mafanikio kutoka ndani ya moyo wangu,” amesema Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani.

“Urafiki wetu hauna mfano pale tunapokabiliana na changamoto zetu kwa kipindi hiki,” alisema Markel katika ujumbe wa Twitter uliotolewa na Msemaji wa Serikali ya Ujerumani.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron ametuma salamu kupitia Twitter kuwa: “Wamarekani wamechagua Rais wao.

Hongera sana @JoeBiden na @KamalaHarris! Tunayo mengi ya kufanya kukabiliana na changamoto za sasa. Tushirikiane!”

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia amempongeza Biden na Harris kwa mafanikio yao ya kihistoria.

“Marekani ni mshirika wetu muhimu na ninatazamia kufanya kazi kwa karibu katika vipaumbele vyetu, kuanzia mabadiliko ya tabia nchi kwenda kwenye biashara na usalama,” alisema Johnson.

Waziri Mkuu wa Ireland, Michael Martin alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza kuandika katika twitter kuhusu uchaguzi. “ napenda kumpongeza Rais mteule wa Marekani @JoeBiden. Joe Biden amekuwa rafiki wa kweli wa nchi yake kipindi chote cha maisha yake na ningependa kufanya naye kati katika kipindi kijacho. Napenda pia kumkaribisha tena nyumbani muda mazingira yatakaporuhusu.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Ugiriki, Kyriakos Mitsotakis kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika: Hongera kwa Rais mteule wa Marekani @JoeBiden. Joe Biden amekuwa rafiki wa kweli wa Ugiriki na ninatumaini kwamba katika kipindi chake urafiki kati ya nchi zetu utashamiri."

Naye Rais wa Iraq, Barham Saleh alituma salamu zake za pongezi akimweleza Biden kama rafiki na mdau wa kuaminika  katika ujenzi wa Iraq iliyo bora. (Tunatazamia kufanya kazi pamoja kufanikisha malengo yetu na kuimarisha amani na usalama katika Mashariki ya Kati.”

Naye Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri, alisema “Misri , ikiwa nchi ya Kiarabu yenye watu wengi, inatazamia kuendelea makubaliano ya nchi yetu na Marekani kwa manufaa ya nchi na zote mbili  na watu wake.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com