WAZALISHAJI WA VIFAA TIBA WATAKIWA KUJALI KWANZA AFYA YA MTUMIAJI KWA KUZALISHA VIFAA TIBA VILIVYOKIDHI VIWANGO VYA UBORA


Afisa Viwango Vifaa Tiba kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Bw.Alexander Mashalla  
************************************
 Wazalishaji na wasambazaji wa vifaa tiba wametakiwa kuzalisha bidhaa hizo zilizokidhi viwango vya ubora ili kuweza kulinda afya ya mtumiaji ili asiweze kudhurika.

 Akizungumza na Mwandishi wetu Jijini Dar es Salaam, Afisa Viwango Vifaa Tiba kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS),Bw.Alexander Mashalla amesema kiwango ambacho kinatumika kudhibiti ubora cha ISO-13485 kinawasaidia wazalishaji na wasambazaji wa vifaa tiba kuweza kukidhi matakwa ya wateja kwa maana wateja wanahitaji bidhaa iliyobora.

 "kutumia kiwango cha ISO-13485 ambacho kinatoa muongozo au mifumo ya usimamizi wa ubora ambao utasaidia kifaa tiba kitakachotumika kiweze kutumika kama inavyopaswa lakini kiwe kimekidhi matakwa ya ubora yanayotakiwa". Amesema Bw.Mashalla.

 Aidha Bw.Mashalla amesema Kiwango hicho wamekipitisha kutokea ISO pia kina namba ya Tanzania ambayo Tzs 1967. Sambamba na hayo Bw.Mashalla amesema miongoni mwa sehemu ya kiwango hicho inaelezea kuhusu matakwa ya kiwango yaani ili mzalishaji au msambazaji wa vifaa tiba anapaswa kufanya nini ili kukidhi matakwa ya kiwango hicho. 

Hata hivyo amesema sehemu nyingine imeelezea wajibu wa uongozi wa taasisi au kampuni inayohusika na uzalishaji au usambazaji wa vifaa tiba kuweka mifumo ya usimamizi wa ubora, namna gani inaweza kuisimamia, namna gani inaweza kuidhibiti. 

Pamoja na hayo Bw.Mashalla amesema wazalishaji na wasambazaji wa vifaa tiba na wataalamu wanaotumika kwenye kusimika vifaa tiba kwenye hospitali pamoja na njia za kuvitupa vifaa tiba baada ya kuisha kwa matumizi wanakuwa wanafuata mifumo inayotambulika ambayo itawasaidia kukidhi matakwa ya kisheria kwenye mamlaka ya kudhibiti ubora.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post