Jeshi la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kuwasaka wanasiasa Halima Mdee na Zitto Kabwe, huku likiwataka wajisalimishe ili wajibu tuhuma zinazowakabili.
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Novemba 3 na Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa imeeleza wanaendelea na opareshini ya kuwakamata watu wanaofanya mipango kuhamasisha maandamano nchini.
Mambosasa ameeleza kuwa hadi sasa jeshi hilo linawashikilia watu 14 wakiwemo viongozi wa Chadema ambao ni Freeman Mbowe, Godbless Leman a Boniface Jacob.
Kamanda huyo ameeleza kuwa hali ya jiji la Dar es Salaam imeendelea kuwa shwari, huku akiwataka wanasiasa kuacha kufanya fujo na badala yake kufuate sheria.
Social Plugin