Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Sweetbert Njewike.
***
Watu 14 wamefariki dunia papo hapo na watatu kujeruhiwa mkoani Singida, kufuatia ajali ya barabarani mara baada ya gari ndogo aina ya Hiace iliyokuwa ikitokea mkoani Mwanza kugongana uso kwa uso na Lori maeneo ya Ikungi mkoani humo.
Akizungumza hii leo Desemba 14, 2020, Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Sweetbert Njewike, amethibisha kutokea kwa ajali hiyo ambapo, waliofariki katika ajali hiyo watu saba ni wanaume na saba ni wanawake na majeruhi wanatibiwa katika hospitali ya wilaya ya Manyoni.
"Chanzo cha ajali ni dereva wa gari lililokuwa linatokea Mwanza kulipita gari lililokuwa mbele yake, bila kuchukua tahadhari na hivyo kusababisha kugongana uso kwa uso na lile Lori lililokuwa linatokea Dar es Salaam kwenda Kahama, waliotambuliwa ni mmoja ambaye ni dereva wa gari ndogo na wote hawa ni wakazi wa Mwanza na ndugu zao taarifa wanazo baadaye watakuja kutambua miili ya ndugu zao", amesema Kamanda Njewike.
Kamanda Njewike ametoa wito kwa madereva kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani, na miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya mkoa wa Singida.
Social Plugin