Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Ofisi ya Rais -Tamisemi, Suleiman Jaffo kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita Mhandisi Modest Aporinary kutokana na matumizi mabaya ya fedha za Serikali Sh Milioni 400 zilizolenga kuhudumia wananchi lakini akanunua gari la kutembelea.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo Jumatano wakati akiwaapisha Mawaziri na Naibu Mawaziri Ikulu Chamwino Dodoma.
“TAMISEMI kuna matumizi mabaya ya fedha Jafo Suleiman Waziri wa TAMISEMI umefanya vizuri sana lakini kwenye kudhibiti fedha bado, nimefikiria sana kukurudisha au kutokukurudisha",amesema Rais Magufuli.
"Hapo nataka kusema ukweli tuelewane hili la matumizi mabaya. Unakuta mkurugenzi ananunua gari la milioni 400 fedha tumehangaika nazo kuzipata wananchi, watoto wanachangishwa unakuta madawa hayatoshi. Nataka kazi yako ya kwanza kwenda kumsimamisha mkurugenzi wa Geita ndiyo kazi yako ya kwanza ukaanze nayo", amesema
Social Plugin