Kampuni ya Vinywaji ya Jambo Food Products imeibuka mshindi wa kwanza kundi la viwanda kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.
Nafasi ya pili imechukuliwa na Kampuni ya Fresho huku nafasi ya tatu katika maonesho hayo ikichukuliwa na Kampuni ya Vijana Foam Manufactures na wote kukabidhiwa vyeti na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kakula wakati akifunga maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini yaliyoongozwa na kauli mbiu ya ‘Biashara na madini ni chachu ya maendeleo Shinyanga’ leo Jumanne Desemba 1,2020.
Mbali na kutangaza vinywaji mbalimbali ikiwemo Juisi, Maji na Soda, Kampuni ya Jambo Food Products pia imetambulisha rasmi Pipi na Biskuti za Jambo.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo, Anwali Saidi ambao ni washindi wa kwanza katika maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini kundi la Viwanda. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo, Anwali Saidi ambao ni washindi wa kwanza katika maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini kundi la Viwanda.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Mhe. Jasinta Mboneko na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela wakiwa katika Banda la Jambo kwenye maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini katika eneo la Butulwa Old Shinyanga wakiwa na Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula (haonekani vizuri pichani).
Kushoto ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo, Anwali Saidi akimwelezea Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula kuhusu bidhaa zinazozalishwa katika Kampuni ya Jambo zikiwemo Juisi, Maji, Soda, Biskuti na Pipi
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo, Anwali Saidi akionesha bidhaa zinazozalishwa katika Kampuni ya Jambo zikiwemo Juisi, Maji, Soda, Biskuti na Pipi
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko akielezea kuhusu Kampuni ya Jambo.
Muonekano wa Banda la Kampuni ya Jambo
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog