Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA AFYA, WORLD VISION WAZINDUA KITENGO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA LISHE HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akisikiliza maelekezo ya mlo bora , kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu -Shinyanga. 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee  na Watoto, kwa kushirikiana na Shirika la World Vision, wamezindua kitengo cha kutolea huduma za lishe katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, ili kutokomeza tatizo la udumavu kwa watoto.


Uzinduzi wa kitengo hicho cha kutolea huduma za lishe umefanyika leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, na kuambatana na zoezi la upimaji afya bure kwa wananchi ili kujua afya zao na kupewa elimu ya lishe ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Masovela. 

Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, amesema tatizo la udumavu mkoani humo bado lipo, na hivyo kuwataka wadau wa afya pamoja na watumishi wa Serikali, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi tena kwa vitendo, namna ya kuzingatia lishe bora. 

Amesema Serikali mkoani humo inaendelea na juhudi za kutokomeza tatizo la udumavu, na ndio maana kwa sasa wameshazindua zoezi la utoaji wa chanjo ya matone ya Vitamini 'A' pamoja na dawa za minyoo kwa watoto, huku akibainisha kuwa wameshaingia mikataba na wakuu wa wilaya, pamoja na wakurugenzi, ili kuhakikisha udumavu una kwisha.

Kaimu Mkurugenzi msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Grace Moshi, akizungumza kwenye uzinduzi huo, amesema suala la kuzingatia lishe dhidi ya watoto wadogo nila muhimu sana, ambapo litawajenga kiakili, na kiafya. 

Amesema mtoto ambaye anazaliwa na udumavu hata kufikiri kwake kuna kuwa kwa kiwango cha chini, na hawezi kuwa mzuri kwenye masomo yake, tofauti na mtoto ambaye hana udumavu ambapo atakuwa mzuri (Bright), na ndiyo maana Serikali imeamua kuwekeza kwenye suala la lishe ili kumaliza tatizo la udumavu hapa nchini. 

“Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe, ili kuhakikisha tatizo hili la udumavu hapa nchini linatokomea kabisa, pamoja na magonjwa mengine ambayo yanasababishwa na ulaji vyakula hovyo bila ya kuzingatia lishe bora,”amesema Moshi. 

Naye Mkurugenzi wa miradi kutoka Shirika la World Vision Nesserian Mollel, amesema Shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi ya lishe kwenye wilaya 36 hapa nchini, zikiwamo na wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga, ambazo ni Kishapu, Kahama Mji, Manispaa ya Shinyanga, na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga. 

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo wa lishe, wanaangalia suala la ulinzi na mazingira ya mtoto, elimu ya mtoto, afya ya mtoto, mahusiano mazuri ya mtoto na mazingira, pamoja na kutoa vifaa tiba ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za afya. 

Aidha Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga Dennis Madeleke, akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa mkoa huo, ametaja hali ya udumavu kuwa ni asilimia 32, na kubainisha kuwa uzinduzi  huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe mkoani humo, utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la udumavu. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akizungumza kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi msaidizi wa huduma za lishe kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto Grace Moshi, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa miradi kutoka Shirika la World Vision Nesserian Mollel, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga Dennis Madeleke, akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa mkoa huo kwenye uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Mzazi Dina Ibrahimu mkazi wa kijiji cha Wisheteleja wilayani Kishapu akitoa ushuhuda namna elimu ya lishe bora ilivyo okoa afya ya mtoto wake, ambaye alizaliwa akiwa na uzito pungufu.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, (kulia), akiwa kwenye chumba cha kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, kushoto ni mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoani Shinyanga yatokanavyo na ulaji holela Ruth Kanoni, akipewa vifaa vya kutolea elimu ya lishe bora.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Zoezi la uzinduzi likiendelea.
Zoezi la uzinduzi likiendelea.
Zoezi la uzinduzi likiendelea.
Bango likiwa kwenye uzinduzi huo.
Afisa lishe Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Saidi Mankiligo, akitoa maelekezo kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, namna ya kuzingatia mlo kamili.
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akisikiliza maelekezo ya mlo bora , kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao bure, pamoja na kupewa ushauri wa kuzingatia lishe bora, kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao bure, pamoja na kupewa ushauri wa kuzingatia lishe bora, kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao bure, pamoja na kupewa ushauri wa kuzingatia lishe bora, kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com