MADIWANI KISHAPU WAAPISHWA , KUANZA NA UJENZI WA SHULE, VYUMBA VYA MADARASA NA MADAWATI

Madiwani wilayani Kishapu wakila kiapo cha kuwa madiwani rasmi, ambao walishinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Na Marco Maduhu, Kishapu 
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, wameapishwa Rasmi na kupewa jukumu la ujenzi wa shule, vyumba vya madarasa, pamoja na madawati, ili kukabiliana na changamoto ya wanafunzi kusoma kwenye miti na kukaa chini.

Zoezi la kuapisha madiwani hao limefanyika Desemba 14,2020 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, lililofanywa na Hakimu Mkazi Mahakama ya Wilaya ya Kishapu Amana Ismail. 

Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, akizungumza wakati wa kufungua zoezi hilo la kuapisha madiwani hao, amesema jukumu la kwanza ambalo wanatakiwa kwenda kuanza nalo ni kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati, ili wanafunzi watakaoanza masomo Mwezi  Januari 2021 wasisome kwenye mazingira ambayo siyo rafiki. 

"Madiwani mmeshakula kiapo leo na kuwa madiwani Rasmi, hivyo nawaomba jukumu la kwanza ambalo mnatakiwa kwenda kulifanya ni kumaliza tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na madawati, ili wanafunzi wasikae chini na kusomea kwenye miti," amesema Kengese. 

Naye Mkuu wa wilaya hiyo ya Kishapu Nyabaganga Taraba akitoa salamu kwenye zoezi hilo la uapisho madiwani, amesema wilayani humo mwakani kutakuwa na idadi kubwa ya wanafunzi, hivyo kuna baadhi ya Kata zinatakiwa kujengwa shule mpya. 

Amezitaja Kata hizo kuwa ni Lagana, Sekebugolo, Isoso, Mwaweja, Shagihilu, Mwasubi, na Bupigi, na kuwataka madiwani hao wakafanye kazi hiyo ya ujenzi wa shule mpya pamoja na ujenzi huo wa madarasa na madawati, kwa kushirikiana na wananchi kuchangia shughuli hizo za maendeleo. 

Nao baadhi ya madiwani hao akiwamo Edward Nkuba kutoka Kiloleli, wamesema watakwenda kulifanyia kazi suala hilo la upungufu wa vyumba vya madarasa, madawati, na ujenzi wa shule, kwa kushirikiana na wananchi, pamoja na Mgodi wa Almas Williamson Diamond. 

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, aliwaomba madiwani kuwa na ushirikiano wa kutosha kwenye ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule, ambapo tayari walikuwa wameshaanza ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye baadhi ya shule. 

Kwa upande Mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, ameahidi ushirikiano na madiwani hao, ambapo Januari 2021 ataanza ziara ya kukagua ujenzi wa miundombinu hiyo ya shule, na kuona namna ya kutatua changamoto zake ikiwamo ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati. 

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI.
Mbunge wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo akizungumza kwenye uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba akizungumza kwenye zoezi la uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, akizungumza kwenye uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, akizungumza kwenye zoezi hilo la Uapisho wa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu William Jijimya, akizungumza mara baada ya kumaliza zoezi la kula kiapo na kupigiwa kura za ndiyo kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Underson Mandia, akizumgunza mara baada ya kumaliza kula kiapo na kupigiwa kura za ndio kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Kishapu Amana Ismail, akiwaapisha Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mara baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakila kiapo cha kuwa madiwani rasmi, mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu wakila kiapo cha kuwa madiwani Rasmi, mara baada ya kushinda kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

Na Marco Maduhu- Kishapu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post