Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAJAMBAZI YAVAMIA VIWANDA MPANDA..YAPORA MIL 15 NA KUKATA MAPANGA WALINZI

NB-Picha haihusiani na habari hapa chini.
**
Walinzi wawili katika viwanda vya kukoboa mpunga vya Mpanda Hoteli Manispaa ya Mpanda, wamekatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili yao baada ya kuvamiwa na majambazi waliofanikiwa kupora Shilingi 15 milioni mali ya mmiliki mmoja wa kiwanda Mashauri Noni.

Inaelezwa kuwa majambazi hao walivamia kiwandani hapo Desemba 13,2020 saa 5:00 usiku kisha kumkatakata kwa mapanga mlinzi wake Abeli Samweli mkazi wa Mpanda Hoteli hali iliyosababisha kulazwa hospitali ya rufaa mkoa wa Katavi.

Jeshi la Polisi mkoani Katavi limethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba wanaendelea na uchunguzi ili kuwabaini watuhumiwa waliohusika na tukio hilo.

Via Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com