Na Grace Mwakalinga, MBEYA
Umoja wa Wanawake wa vyombo vya ulinzi na usalama Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya, ukiongozwa na Mwenyekiti wao Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polise A.S.P Janeth Masangano wametoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa waliopo kwenye hospitali ya Wilaya.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ambao umegharimu kiasi cha shilingi 650, 000/=, ASP Janeth Masangano amesema miongoni mwa misaada hiyo ni pamoja na ma mashuka ya MSD sabuni za maji lita ndoo za kufanyia usafi, Sabuni za kufulia, mafuta ya kupaka, juisi na biskuti.
Masangano amesema msaada huo ni sehemu ya kuisaidia wagonjwa ambao walifanyiwa vitendo vya ukatili.
“Tumeguswa na yanayowakuta wenzetu ndio maana tumeamua kuja kutoa msaada wakati tunaendelea na maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ambazo zinamlenga mwanamke moja kwa moja kwa kuwa yeye ndie mhanga wa vitendo vya ukatili, zaidi kwa watoto na akinamama ambao wametoka kujifungua.”
Pia amewasisitiza kina mama kuongeza umakini kwa watoto hasa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu.
Katibu wa umoja huo SP Yusta Mdegela amesema Wanawake wanapaswa kukemea na kuripoti vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutoa taarifa kwenye vyombo vya usalama ili sheria ichukue mkondo wake.
Akiongea kwa niaba ya watumishi wa Afya Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Dr. Azaer Luvanda ameushukuru umoja huo kwa kuwatembelea wagonjwa hospitalini sambamba na kutoe elimu kwa Wanawake