Na Dinna Maningo - Malunde 1 Blog
Wanandoa nchini wametakiwa kupendana na kusikilizana kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza nguvu zinazotumiwa na wanaume katika kurekebisha makosa ya wake zao.
Hayo yalielezwa na wana kundi la "CCM No.1" wakati wa mjadala wao kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp kundi lenye wajumbe 203 kutoka mikoa mbalimbali nchini Tanzania.
Mjadala huo ulihusu kutaka kufahamu ni kwa namna gani wanaume watumie njia nzuri katika kurekebisha makosa ya wake zao badala ya kutumia nguvu ambazo wakati mwingine ni za uonevu.
Mjadala ulikuwa na maswali manne ya kichokozi yaliyolenga kufahamu, "Je ni kweli wanaume utumia nguvu kubwa katika kurekebisha
makosa ya wake zao?"
,Je unafikiri ni nguvu zipi zinazoonekana kutumiwa na wanaume ambazo unaona ni uonevu kwa mwanamke?
Je unafikiri ni kwanini wanaume wanatumia nguvu katika kurekebisha makosa ya wake zao? na unafikiri ni njia zipi na nzuri ambazo wanaume wanaweza kuzitumia kama suluhisho katika kurekebisha makosa ya wake zao ambazo si za nguvu na uonevu?.
Newton Mwongi kutoka mkoa wa Mara alisema kuwa suluhisho la mme kurekebisha makosa ya mke wake si kwa kutumia nguvu bali ni mme kupata muda wa kukaa na mke wake na kumsikiliza pamoja na kudumisha upendo kwa wanandoa na kuishi na mke wako kama rafiki yako namba moja ndiyo suluhisho la uhimarifu wa ndoa na siyo kumpiga na kumnyanyasa huku Yugen Kyaro kutoka Mara akiwataka wanandoa kukaa pamoja kuelezana pindi mwenza wake anapomkosea.
Juliet Ghati kutoka Mara alisema kuwa ni kweli baadhi ya wanaume utumia nguvu katika kurekebisha makosa ya wake zao huku akitaja baadhi ya nguvu zinazotumika.
"Kuna kupigwa,kufukuzwa nyumbani, kunyimwa haki za msingi kama wanandoa na hata matusi na vitendo vya udharirishaji,wanaume wanatumia nguvu kurekebisha makosa kwa sababu wengine ni asili yao na akili walizonazo hawaamini kama kuna njia nyingine ya kutatua tatizo bila kutumia nguvu!mfano unaishi na mvuta bangi,mtumiaji wa pombe kupitiliza,jambazi na tabia za aina hiyo huyo hawekuamini njia nyingine zaidi ya kutumia nguvu.
"Tabia zetu sisi wanawake na ulimbukeni wetu wa kuiga tamaduni ambazo siyo zetu,mfano unakuta mwanamke umekisea na hutaki kushuka wala kukiri kosa,umejaza maneno machafu mdomoni,unamropokea ovyo mmeo unaweza kusababisha hasira na kumfanya akuadhibu bila kutarajia,lakini pia wakati mwingine tunashindwa kusimama katika nafasi zetu kama wanawake na kusababisha kero na uchungu kwa wenzetu", alisema Ghati.
Ghati aliongeza kuwa njia nzuri ambazo wanaume wanaweza kuzitumia kurekebisha makosa ni kuijua tabia halisi ya mkeo,madhaifu yake na vitu anavyovipenda kisha kaa naye,mshauri,mwelekeze na mjadili mapungufu yaliyopo kwa mapenzi bila kuonyesha chuki wala hasira na umchukulie mwenzi wako sawa na ndugu yako hata kama amekosea.
"Sidhani kama kuna mtu atafurahi kumuona ndugu yake katika shida, hata kama ana mapungufu huwa tunavumilia,mvumilie na mkeo pamoja na mapungufu yake,ukishindwa usitumie nguvu sana yeye ni mtu mzima tafuta suruhu bila kuleta madhara", alisema Ghati.
Ghati aliwashukia wanawake na kusema"Matatizo mengine tunayasababisha wanawake wenyewe,hata wanaume pia wanavumilia mengi toka kwetu hivyo tusifikiri wao wameridhika na hali zao.Tuvumiliane na tusikurupuke na tamaduni za nje tukasahau zetu!.
"Haya mambo ya haki za wanawake yametufanya wababe sana na kuleta matatizo makubwa kwa baadhi ya wenzetu! kila mmoja kwa nafasi yake amuheshimu mwenzake na atambue jukumu na wajibu wake kwenye familia mambo yataenda,nguvu zingine huzisababisha sisi wanawake kutumika kwa tabia na matendo yetu kwa wenzetu",alisema Ghati.
Acren Shaibu kutoka Mara alisema "Hakuna mkate mgumu mbele ya chai mwanamke ukitambua wajibu wako na kuutekeleza vizuri kabisa vipigo na manyanyaso utavisikia kwa jirani tu,"Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa"hakuna haki bila wajibu mara nyingi tunasikia matangazo ya zijue haki za mwanamke lakini hatusikii ujue wajibu wa mwanamke.
Aliongeza"Kinachopelekea mambo yanakuwa magumu hadi kuanza ugomvi, wanawake wengi wamekuwa ni wanaharakati na sio wake za watu tena, turejee kwa bibi zetu waliishii vipii? Je hakukuwa na haki?
mbona mambo haya yamezidi sana kwenye kizazi hiki! ninachokiamini haki ya mwanamke ipo pale pale kama mwanamke atajitambua na kutimiza wajibu wake ipasavyo",alisema Shaibu.
Lucas Kilima yeye alisema kuwa "Nguvu inayotumika ni kipigo huku sisi tukiamini kama njia sahihi ya tiba kwa wake zetu na hasa kwetu sisi wakurya tukiwa tunatumia lugha fulani kuwa mwanamke kama humpigi humpendi.
"Nakumbuka ilikua mwaka 2015 katika kijiji cha Muriba niliwahi kumsikia mwamke mmoja akisema yeye bila kupigwa na mmewe hampendi na akaenda mbali zaidi na kusema huwa anamchokoza mme wake ili ampige ajue anapendwa",alisema Kilima.
Yugen Kyaro kutoka Mara alisema kuwa wanawake wa Kikurya bila kumpiga atakudharau japo sio wote lakini Oliver Nyamanche kutoka Mara alipinga na kusema si kweli na Patricia Kabaka kutoka Dodoma alisema;
"Siamini kama kuna mtu katika karne hii ana mtazamo kama huo siku zote naamini huu msemo ni kuendelea kuwadidimiza wanawake wa kikurya ili waone kupigwa ni moja ya haki yao katika ndoa na siamini kama kuna mwanamke yeyote hata kama sio mkurya anapenda apigwe ndio ajiskie kupendwa, kwanza ni udhalilishaji kwa sisi wanawake wote wa kikurya!" alisema Kabaka.
Veronica Merengo kutoka Mara alisema kuwa hizo ni hisia binafsi na mtazamo hasi huku Mwongi akihoji kuwa kipigo ndio suluhisho?na Kilima akijibu kuwa kipigo sio suluhisho bali ni unyanyasaji,Mwongi akisisitiza kuwa tamaduni zetu zinachangia Sana kuimarisha unyanyaji.
Pili Chacha kutoka Mara alisema"Wanaume hata kama wanateseka wakae kimya walitutesa sana ni zamu yetu na sisi tulipize, wanawake tukipata nafasi ya kufidia unyanyasaji wa vipigo na hasa ubakaji(kwenye ndoa)unapambana naye na kisawasawa".
Dickson Christopher alisema kuwa mwanaume kutumia kiboko ama nguvu inatokana na mke anavyoishi na mme wake kwani baadhi ya wanawake ni wakorofi kupindukia na wenye viburi.
Aliongeza kuwa hakuna mwanaume anayeweza kumpiga mwanamke pasipo makosa nakwamba kuna wanaume wengine upigwa na kuteswa na wake zao japokuwa wanaume hawatoi siri ya manyanyaso wanayopata na wengine kunyimwa tendo la ndoa.
Social Plugin