Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWILI WA MFANYABIASHARA MAARUFU SUBASH PATEL KUZIKWA KESHO DAR

Subhash Patel, enzi za uhai wake.
Subash Patel , enzi za Uhai wake.

Mwili wa mfanyabiashara maarufu Mwenyekiti Mtendaji wa Motisun Group Subash Patel ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) Subash Patel utazikwa kesho katika makaburi ya Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Akitoa ratiba ya shughuli nzima ya kuaga pamoja na mazishi Msemaji wa Makampuni ya Motisun Group, Bw. Aboubakari Mlawa amesema kuwa marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na ameacha mke mmoja pamoja na Watoto wawili.

Bw. Patel alifariki dunia usiku wa kuamkia jana akiwa nyumbani kwake, Kisutu Jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiendelea na matibabu.

Mfanyabiashara huyo maarufu nchini alikuwa akimiliki kampuni zinazotengeneza bidhaa za plastiki, saruji, mabati, nondo, nyaya za umeme, vinywaji, rangi na pia alimiliki hoteli za White Sands na Sea Cliff, Pearlsun Hotel & Resorts.

Via EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com