KAMPUNI YA SHINYANGA BEST IRON YASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOJIA YA MADINI

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Uundaji wa Vifaa vya Uchimbaji na Uchenjuaji Madini ya Shinyanga Best Iron imeshiriki katika Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Novemba 28,2020 katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 

Akizungumza leo Desemba 1,2020 wakati Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akifunga Maonesho hayo, Mkurugenzi wa Kampuni ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula amesema wametumia fursa ya maonesho kuonesha namna wanavyofanya kazi. 

Salula amesema kampuni yao inajihusisha na masuala ya uchomaji na ubunifu,uundaji wa mashine za nafaka ‘vinu’,ufundi wa mitambo ya viwandani,zana za mgodini na matengenezo mbalimbali. 

Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula ameipongeza Kampuni hiyo kwa ubunifu walionao na kuwaomba kuangalia namna ya kuwapatia vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji wachimbaji wadogo wa madini ili kurahisisha kazi za uchimbaji. 

Naye Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Said Pamui amesema atakutana na Kampuni ya Shinyanga Best Iron ili kujadili namna ya kuwakopesha vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji madini wachimbaji wa madini huku akisisitiza umuhimu wa wachimbaji wadogo wa madini kutumia huduma za kibenki badala ya kutembea na fedha ama kutunza fedha majumbani. 
Kulia ni Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuundaji wa Vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula Gacha katika viwanja vya Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga katika eneo la Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. 

Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuundaji wa Vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula Gacha akieleza shughuli zinazofanywa na Kampuni hiyo ambayo pia inafanya kazi ya uchimbaji Madini.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akiipongeza Kampuni ya Uuundaji wa Vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji madini ya Shinyanga Best Iron kwa shughuli inazozifanya
Rais wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo Tanzania (FEMATA), John Bina  akizungumza katika banda la Shinyanga Best Iron.
Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini Tanzania Prof. Idris Kakula akitoa zawadi ya cheti kwa washiriki wa maonesho ya Biashara na Teknlojia ya Madini, kushoto ni Mkugenzi wa Kampuni ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula Gacha
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui (kulia) akitembelea banda la Kampuni ya Shinyanga Best Iron. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uuundaji wa Vifaa vya uchimbaji na uchenjuaji madini ya Shinyanga Best Iron, Kashi Salula Gacha  akimwelezea Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Said Pamui jinsi wanavyofanya kazi.
Sehemu ya Banda la Shinyanga Best Iron

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post