Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Henry Tandau akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wana Olimpiki Tanzania (TOA), katika ukumbi wa Dodoma Hotel, jijini Dodoma leo Desemba 10, 2020. Tandau alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo ambapo wajumbe TOA watashiriki kuchagua viongozi wao wapya. Kushoto ni Rais wa TOA, Gidamis Shahanga na kulia ni Katibu Mkuu wa TOA, Mwinga Mwanjala. Picha na Richard Mwaikenda
Rais wa Chama Cha Wana Olimpiki Tanzania (TOA), Gidamis Shahanga akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Makamu wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Tandau kufungua mkutano mkuu wa TOA.
Social Plugin