UDIDA YAFANYA MKUTANO MKUU WA MWAKA, MEYA NKULILA AAHIDI USHIRIKIANO NA WADAU WA MAENDELEO

 

Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia UDIDA Jasson Kyaruzi, kutokana na ushirikiano wake aliouonyesha tangu Asasi hiyo ilivyokuwa changa mpaka sasa ina mafanikio makubwa ikiwemo kumiliki ofisi.

Na Marco Maduhu  -Shinyanga. 
Asasi ya kiraia UDIDA ambayo inajishughulisha na shughuli mbalimbali zikiwemo za kijamii, imefanya mkutano wake mkuu wa mwaka, kwa kujadili mambo mbalimbali zikiwemo huduma za kijamii. 

Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Ofisi wa Asasi hiyo iliyopo katika Mtaa wa Butengwa -Ndembezi, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila. 

Mkurugenzi wa Asasi hiyo Jasson Kyaruzi, amesema wamefanya mkutano huo wa mwaka, ili kujadili mambo mbalimbali ikiwamo kupanga mikakati ya mwaka (2021), namna watakavyofanya kazi pamoja na kupanua wigo wa huduma zao, ili kusaidiana na Serikali kusukuma gurudumu la maendeleo katika mji wa Shinyanga. 

“Matarajio yetu ya mwaka 2020 ni kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wa maendeleo, kwa ajili ya kuhudumia wananchi kwenye mahitaji mbalimbali, huduma ambayo tumekuwa tukiifanya ndani ya jamii kama sehemu ya majukumu yetu,”amesema Kyaruzi. 

“Mfano kwa mwaka huu tumetoa msaada katika shule ya msingi Buhangija yeye watoto wenye uhitaji, kituo cha watoto wenye mtindio wa ubongo, kituo cha kulea watoto waliofanyiwa ukatili cha Agape APC, pamoja na kutoa msaada wa mifuko ya Saruji katika shule ya Sekondari Town,”ameongeza Mkurugenzi huyo. 

Pia amesema mbali na shughuli hizo za kijamii, pia Asasi hiyo ndani yake ina chama cha kukopeshana (SACCOS), ambayo ina wanachama 80, wanaume 58, na wanawake 22, ambao wana hisa za shilingi Milioni 36, ambapo matarajio yao makubwa ni kupanua wigo zaidi kwa kuongeza wanachama wapya. 

Kwa upande wake mgeni rasmi Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, ameipongeza Asasi hiyo ya UDIDA , pamoja na wanachama wake wa SACCOS kwa kazi nzuri wanayoifanya ikiwamo ya kusaidia jamii katika utoaji wa misaada mbalimbali, na kuahidi Serikali itashirikiana nao pamoja na wadau wengine wa maendeleo. 

Aidha ametoa nasaha kwao waendelee kuwa na nidhamu, uwajibikaji, umoja, mshikamano, pamoja na kusikilizana, ili waweze kusonga mbele pamoja na kufikia malengo yao, huku akiwataka wafikirie pia wazo wa kuanzisha Benki yao na siyo kuishia SACCOS tu, ili wakue kiuchumi na kuweza kusaidia jamii vizuri. 

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulia, akizungumza kwenye mkutano mkuu wa UDIDA.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila akiendelea kusisitiza jambo kwenye mkutano mkuu wa UDIDA.
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia (UDIDA) Jasson Kyaruzi akizungumza kwenye mkutano mkuu wa UDIDA.
Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia (UDIDA) Jasson Kyaruzi akiendelea kuzungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Butengwa Onesmo Mahenza, akizungumza kwenye mkutano huo.
Afisa kutoka Shirika la AGPAHI, Kassabrankahr Herman, akizungumza kwenye mkutano huo.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Wajumbe wakiwa kwenye mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, (kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia UDIDA Jasson Kyaruzi, kutokana na ushirikiano wake aliouonyesha tangu Asasi hiyo ilivyokuwa changa mpaka sasa ina mafanikio makubwa ikiwemo kumiliki ofisi.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila, (kushoto) akimkabidhi zawadi na cheti Mkurugenzi wa Asasi ya kiraia UDIDA Jasson Kyaruzi kutokana na kazi nzuri ambayo anaifanya.
Zoezi la utoaji Zawadi na cheti likiendelea kwa watumishi ambao wamefanya kazi vizuri na UDIDA.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.
Zoezi la utoaji zawadi na cheti likiendelea.

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post