WANAFUNZI SHULE YA MSINGI KEWAMAMBA WAANZA KUPATA UJI SHULENI


Meneja mradi wa  Kituo cha Kilimo Mogabiri  mradi ambao pia unatoa elimu ya Usalama wa chakula katika Jamii chini ya  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Roselyne Mosama akikabidhi vifaa hivyo kwa mmoja wa wanafunzi Shule ya msingi Kewamamba  ili kuanzisha upatikanaji wa uji shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao
***
Na Frankius Cleophace - Tarime.

Suala la upatikanaji wa uji mashuleni bado ni changamoto kubwa katika shule za msingi kwani suala suala  upatinaji wa uji huo linatajwa kuchochea ufaulu kwa wanafunzi hivyo wazazi na walezi hawana budi sasa kuunga mkono juhudi za taasisi zinazojitoa ili huduma hiyo kupatikana.

Shule ya msingi Kewamamba iliyopo wilayani Tarime Mkoani Mara  sasa inaanza kunufaika na Mradi wa upatikanaji wa uji mashuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.

Meneja mradi wa  Kituo cha Kilimo Mogabiri  mradi ambao pia unatoa elimu ya Usalama wa chakula katika Jamii chini ya  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Tarime, Roselyne Mosama akikabidhi vifaa zikiwemo sufuria, ndoo, vikombe na jagi  ili shule ianze kupika uji  alisema kuwa lengo la kutolewa kwa vifaa hivyo ni kuhakikisha ufaulu unaongezeka kwa wanafunzi hao.

“Tunajua wanafunzi wanatembea umbali mrefu kuja shuleni wanashinda njaa pia kuna baadhi yao wanauwezo wa kupata chakula lakini wengine hakuna tumeanzisha mradi huu kusaidia shule zetu pia mradi huu umeanza mwaka 2017”, alisema Mosama.

Mosama aliongeza kuwa licha ya Shule ya Msingi Kewamamba kupata mradi huo pia shule ya Msingi Abainano inanufaika pia na mradi wa utoaji wa uji shuleni lengo ni kusaidia watoto wote kupata uji na kuongeza ufaulu.

Pia Mosama aliongeza kuwa licha ya kutoa msaada wa vifaa hivyo wamekuwa wakianzisha mashamba darasa ili shule hizo ziweze kuzalisha chakula kwa ajili ya matumizi ya shuleni.

“Tunafundisha jinsi la kilimo bora cha Migomba, Viazi na mbaogamboga lengo ni kuzalisha chakula na kukitumia shuleni au kuuza kwa ajili ya kupata fedha za kulipa mpishi”,alisema Mosama. 

Kwa upande wake Mwalimu mkuu shule ya Msingi Kewamamba pamoja na Wanafunzi na wazazi wanatoa shukrani zao kwa Mradi huo ambapo wazazi wamehaidi kushirikiana vyema ili kuendeleza  mradi wa upatikanaji wa uji shuleni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post