VINARA, Yanga SC wameendeleza rekodi ya kupoteza mechi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya leo kulazimisha sare ya 1-1 na wenyeji, Tanzania Prisons Uwanja wa Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.
Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 44 baada ya kucheza mechi 18 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tisa zaidi ya mabingwa watetezi, Simba SC ambao hata hivyo wana mechi tatu mkononi.
Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza, Tanzania Prisons wakawashitua Yanga SC kwa bao la Jumanne Elfadhili dakika sita tu ndani ya kipindi cha pili akimalizia kazi nzuri ya Nurdin Chona.
Pilikapilika za Yanga zikafanikiwa kuzaa matunda dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho, mkombozi akiwa na mchezaji mpya kutoka Burundi, Said Ntibanzokiza.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Polisi Tanzania bao pekee la Ismail Aziz dakika ya 88 Uwanja wa Chuo cha Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Pamoja na ushindi huo, Azam FC inayofundishwa na kocha wa zamani wa Yanga SC,Mzambia George Lwandamina inabaki nafasi ya tatu na pointi zake 32 baada ya mechi 17.
Uwanja wa Mkwakwani Jijini, bao la dakika ya 76 la Rashid Chambo likawanusuru wenyeji, Coastal Union kulala mbele ya Namungo FC ya Ruangwa mkaoni Lindi iliyotangulia kwa bao la Iddi Kipagwile dakika ya 10 timu hizo zikitoa sare ya 1-1.
Kikosi cha Tanzania Prisons kilikuwa; Jeremiah Kisubi, Michael Mpesa, Benjamin Asukile, Vedastus Mwaihambi, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Salum Kimenya/Ezekia Mwashilindi dk71, Lambert Sibiyanka, Mohammed Mkopi/ Kassim Mdoe dk80, Samson Mbangula na Jeremiah Juma/Marco Mhilu dk9-+4.
Yanga SC; Metacha Mnata, Kibwana Shomari, Yassin Mustapha, Lamine Moro, Bakari Mwamnyeto, Mukoko Tonombe, Tuisila Kisinda, Feisal Salum, Michael Sarpong, Said Ntibanzokiza/Waziri Junior dk86 na Farid Mussa/Deus Kaseke dk61.
CHANZO - BINZUBEIRY BLOG
Social Plugin