Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking News : MWANAMKE AJIFUNGUA KUKU KIGOMA


Muonekano wa kuku anayedaiwa kuwa katika mfuko wa uzazi wa mwanamke huyo.

Na Rhoda Ezekiel  - Malunde 1 blog Kigoma
Mwanamke mmoja Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, amejifungua kuku katika kituo cha Afya Uvinza baada ya kufika kituoni hapo akidai anapata maumivu ya tumbo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Simon Chacha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema tukio hilo limetokea leo asubuhi Jumapili Disemba 6, 2020  baada ya mama huyo kufika katika kituo cha afya akiwa na mume wake akiwa na maumivu ya tumbo.

 "Baada ya muda wauguzi walitoa kuku katika sehemu ya uzazi ya Mama huyo ambapo hakuna damu zilizoendelea kutoka zaidi ya uchafu tu unaotoa harufu mbaya",amesema.

Amesema tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa vipimo vinaonyesha mama huyo hakuwa na dalili yoyote ya ujauzito na haoneshi kama alikuwa na ujauzito na baada ya kutolewa kuku huyo ameendelea kutoa harufu mbaya katika sehemu hiyo ya uzazi na alikuwa na homa.

Hata hivyo amemuagiza mganga mfawidhi ampeleke hospitali ya Rufaa Maweni kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.

"Mama huyu haoneshi dalili zozote ya kwamba alikuwa na ujauzito cha kushangaza zaidi kiumbe hicho hakiusiani na mfuko wa uzazi isipokuwa baada ya vipimo imeonekana mama huyo ana uvimbe kwenye kizazi mpaka sasa tumewasiliana na vyombo vya usalama kufuatilia tukio hilo", amesema Dk. Chacha.

Kwa upande wake Mama huyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, amesema alianza kujisikia maumivu tumboni na hakuwa na dalili zozote za mtu mwenye mimba ameshangaa baada ya kufika Hospitali hapo kutolewa kuku tumboni mwake jambo ambalo pia limemuogopesha.

 Taarifa zisizo rasmi zinasema kwamba mama huyo aliingiziwa kuku huyo na Mganga wa kienyeji.

Nao baadhi ya Wananchi Wilayani humo akiwemo Riziki Mbonabucha wamesema tukio hilo limewashangaza sana maana halijawahi kutokea katika Wilaya ya Uvinza na kama kuna mtu anahusika na kumfanyia kitendo hicho mwenzake achukuliwe hatua ili iwe fundisho.

Amesema kazi ya Waganga wa kienyeji ni kuwaondolea Wananchi matatizo na sio kuwaongezea matatizo anashangaa kuona Mganga huyo aliyekosa roho ya huruma kukubali kumuwekea mwanamke kuku tumboni akidai ni unyama unaohitajika kukomeshwa.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kigoma James Manyama kuwa kuku aliyekutwa kwenye kizazi cha mwanamke mkoani humo atapelekwa kwenye Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya kuchunguzwa kwani si kawaida kwa binadamu kujifungua kiumbe cha namna ile.

"Kwa kuwa tukio hili siyo la kawaida kwenye jamii, jeshi la polisi tutachukua kiumbe hicho kwa ajili ya kupeleka Maabara ya Mkemia wa Serikali kwa ajili ya uchunguzi zaidi kwani siyo kawaida kwa binadamu kujifungua kuku", amesema Kamanda Manyama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com