Jumbe mbalimbali zikionyeshwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga Ukatili wa kijinsia leo jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsi Lilian Liundi akingea katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili zilizofanyika viwanja vya Mabibo jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsi Lilian Liundi akingea katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili zilizofanyika viwanja vya Mabibo jijini Dar es salaam.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda akitoa neno katika maadhimisho hayo ambapo alikuwa mgeni rasmi.
Darius Damas ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto idara kuu ya Maendeleo Dk. John Jingu akiongea katika maadhimisho hayo.
**
Na Frankius Cleophace Dar es Salaam.
Asilimia 40 ya Wanawake wenye Umri wa Miaka 15-49 wanatajwa kufanyiwa Ukatili wa kijinsia vikiwemo vipigo pamoja na ukatili wa kingono katika Maisha yao.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu mwaka 2015-2016 kupitia taarifa ya idadi ya watu afya.
Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda ametaja takwimu hizo leo katika maadhimisho ya siku16 za kupinga Ukatili wa kijinsia ambapo alisema kuwa takwimu hizo zinaonyesha kuwa Ukatili bado upo na unaendelea kuongezeka ambapo Mikoa ya Kagera, Mara, Mwanza na Kigoma.
“Kwa ujumla taarifa hiyo inayonyesha hakuna mabadiliko na mitazamo katika jamii zetu hivyo sasa tuendelee kujenga uelewa wa pamoja ikiwemo mahala pa kazi ili kutokomeza pia rushwa ya ngono”, alisema Makinda.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Aseny Muro alisema kuwa lengo la maadhimisho ya Siku 16 ni kuendelea kushawishi serikali ili kuweka mipango ya kuendelea kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo kupangwa kwa bajeti zenye mlengo wa kijinsia.
Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP Lilian Liundi alisisitiza suala la kuendelea kutolewa kipaumbele katika suala la kupinga Ukatili kama ilivyokuwa kwenye janga la Virusi vya Corona.
“Mkurugenzi wa UN WOMEN Duniani alivyokuwa akitoa hotuba yake alisema naiweka kwa kifupi kama juhudi zilizofanyika kwenye janga la Corona kila mtu akasimama, akatafakari zingetumika kwenye kutomeza ukatili wa kijinsia ambao unaruisha uchumi wetu Nyuma, Unadhalilisha Unaua, unapoteza Maisha ukatili ungekuwa umeishaisha”, alisema Lilian.
Kwa upande wake Darius Damas ambaye ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkuu na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Idara kuu ya Maendeleo Dk. John Jingu akieleza mikakati ya serikali alisema kuwa mpaka sasa serikali imeweka mpango kazi wa kutomeza ukatili wa kijinsia mpaka asilimia 50 ifikapo2020-2022 ambapo kamati za kutomoeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto zimeanzishwa 16,343 katika ngazi zote hapa nchini.
"Pia Madawati ya polisi 220 yanayoshugulikia ukatili yameanzishwa , Madawati 161 jeshi la Magereza yameanzishwa na matadawi 05 vyuo vya elimu ya juu na elimu ya kati na kati na shule za Msingi Madawati 155 ya jinsia kutoka Halmashauri 24 na tunatarajia kuwa na madawati katika shule zetu hapa nchini", alisema Darius.
Kauli mbiu ya Mwaka huu katika kampeni ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia inasema kuwa 'Miaka 25 ya Beijing Wekeza, Wezesha, Tokomeza, Ukatili Mabadiliko yanaanza na mimi".