Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mh Josephat Maganga (katikati) akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maduka matatu ya kampuni ya GSM Group mjini Dodoma hivi karibuni. Aliyesimama kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM Tanzania, Bi. Fatma Abdallah na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mh. Anthony Mavunde. Uzinduzi huo ni sehemu ya jitihada endelevu za kampuni ya GSM Group kuendelea kutoa huduma na bidhaa bora kwa wateja wake kutoka sehemu mbalimbali ikiwemo mikoa ya jirani na Dodoma.
Dodoma, 11 Desemba 2020: Kampuni ya GSM Group leo imezindua maduka makubwa eneo la Capital City Mall jijini Dodoma yatakayokuwa yakiuza bidhaa mbalimbali zikiwemo samani za majumbani, maofisini pamoja na mavazi.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa maduka matatu ya kampuni hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa GSM, Bi Fatma Abdallah amesema; GSM inajivunia kusogeza huduma zenye ubora kwa wakazi wa jiji la Dodoma na majirani.
“Kwa kutambua umuhimu na ukuaji wa kasi wa jiji la Dodoma, kampuni ya GSM Group inajivunia hii leo kuzindua maduka matatu yenye bidhaa zenye ubora wa aina yake hapa katika makao makuu ya nchi, “amesema Bi Fatma.
“Sote ni mashahidi kwamba GSM imekuwa ikitoa huduma zenye ubora wa hali ya juu katika maduka yetu mbalimbali yaliyoko jijini Dar es Salaam na kwingineko. uwepo wetu hapa leo ni ishara kwamba jiji la Dodoma limekua na lina hadhi ya kuwa na maduka ya aina hii,” ameongeza.
“Maduka matatu tunayoyazindua hapa hii leo ni GSM HOME, BABYSHOP pamoja na SPLASH. Maduka haya yatakuwa yakitoa huduma za samani za majumbani pamoja na mavazi ya kisasa kwa watu wa rika zote. Hivyo basi napenda kuchukua fursa hii kuwakaribisha wateja wetu wa mkoani Dodoma na mikoa ya jirani kufika katika maduka yetu haya ya kisasa kabisa ili waweze kujipatia bidhaa za kipekee na zenye ubora wa hali ya juu.” Bi, Fatma alifafanua.
GSM inajivunia kuwa na makampuni mengi yakifanya kazi hapa nchini na nje ya nchi. Hii ni awamu ya nne ya bidhaa / huduma za GSM kupatikana hapa jijini Dodoma ambapo awamu ya kwanza tulianza na biashara za bidhaa kama magodoro, vifaa vya ujenzi, betri ndogo na za magari, hamira na GSM coconut. Awamu ya pili tulileta huduma ya usafirishaji wa mizigo mikubwa ndani na nje ya nchi. Awamu ya tatu tukafungua maduka ya mavazi pale Shoppers plaza ikiwemo Max, Shoexpress Pamoja na Homebox. Na sasa awamu hii ya nne tumekuja tena na maduka haya ya nguo pamoja na Samani, yaani Furniture.
Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Dk Bilinith Mahenge, mgeni rasmi katika uzinduzi wa maduka hayo, amewashukuru GSM na kuwapongeza kwa uamuzi wao wa kufungua maduka hayo makubwa na hivyo kulifanya jiji la Dodoma kuwa la kisasa zaidi. “Kwa kutambua umuhimu na ukuaji wa kasi wa jiji la Dodoma, ndiyo maana kampuni kubwa ya GSM Group imeamua hii leo kuzindua maduka matatu hapa kwetu,” alisema.
“Kama kiongozi katika mkoa huu wa Dodoma napenda kuwahakikishia GSM kuwa wamefanya uamuzi sahihi na kwa wakati muafaka. Mimi na wakazi wengine wa hapa ni watumiaji wazuri wa bidhaa zenu ila kwakuwa tulikuwa tunalazimika kuzifuata jijini Dar es Salaam, kidogo ilikuwa inatupa ugumu, tunashukuru kwa kutusogezea huduma hii hapa mlangoni,” Dk Mahenge aliongeza.
Akizungumzia fursa za uwekezaji katika jiji la Dodoma, Dk Mahenge amesema, “Serikali ya awamu ya tano ikiongozwa na Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli imejidhatiti kuhakikisha kuwa wawekezaji wote wanapata mazingira bora kabisa ya uwekezaji. Tumeondoa urasimu na milolongo mingi tukiamini kwamba kufanikiwa kwa mwekezaji, ni kufanikiwa kwa watanzania na Taifa kwa ujumla”
GSM Group ina maduka makubwa yanayouza bidhaa za aina mbalimbali zikiwemo fenicha za kisasa, nguo za jinsia mbalimbali na rika zote, vifaa vya michezo, umeme, magodoro na nyinginezo, zikiwa kwenye ubora wa hali ya juu kabisa. Vyote hivi kwa sasa vitakuwa vinapatikana katika maduka ya GSM yaliyopo Dodoma na jijini Dar es Salaam.
Kwa taarifa zaidi, wasiliana na:
Allan Chonjo
Afisa Biashara Mkuu – GSM Group of Companies
+255 658 450 010
Social Plugin