Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAHAKAMA YATENGUA HUKUMU YA AY, MWANA FA DHIDI YA TIGO


Mahakama Kuu hapa nchini, imetengua hukumu ya wanamuziki wa Bongo fleva Hamisi Mwinjuma (Mwana FA) na Ambwene Yesaya (AY), iliyoamuru kulipwa Shilingi Bilioni 2.1 na kampuni ya simu za mkononi ya Tigo baada ya kampuni hiyo kukiuka sheria za hatimiliki.

Jaji Joacquine wa Mahakama hiyo De-Mello amekubaliana na rufaa ya kampuni ya Tigo kuwa mahakama ya wilaya ya Ilala haikuwa na mamlaka ya kisheria kusikiliza kesi hiyo.

Tayari kampuni hiyo ya simu za mkononi ya Tigo iliishawalipa Mwana FA na AY fedha hizo kiasi cha shilingi bilioni 2.1.

Mwezi Aprili 2016, Hakimu Mkazi Mwandamizi wa mahakama ya wilaya ya Ilala, alitoa amri ya Wanamuziki hao kulipwa kufuatia kesi ya madai waliyoifungua dhidi ya kampuni ya Tigo.

Wakili wa kampuni ya Tigo, Rosan Mbwambo amesema atawaandikia barua Wanamuzìki hao kuwataka warejeshe fedha walizolipwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com