Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Jijini Dodoma Kusaya amesema maonesho haya yatakuwa ni ya 29 tangu yalipoanza kuadhimishwa mwaka 1993 na kuwa Wizara ya Kilimo inatoa wito kwa wadau wote wa maonesho zikiwemo Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri, Taasisi za umma na binafsi, wakulima, wafugaji, wavuvi na wanaushirika kuanza maandalizi ya kufanikisha maonesho.
Pamoja na kufanyika kitaifa mkoani Tabora, Maonesho yatafanyika pia kwenye Kanda zingine (7) ambazo ni Kanda ya Mashariki Uwanja wa Maonesho ya Mwl. Nyerere (Morogoro); Kati (Nzuguni - Dodoma); Kusini (Ngongo – Lindi); Nyanda za Juu Kusini (John Mwakangale – Mbeya); Kanda ya Ziwa Mashariki (Nyakabindi – Simiyu); Kanda ya Ziwa Magharibi (Nyamhongolo –Mwanza), na Kaskazini (Themi – Arusha).
Imetolewa na:
Revocatus A. Kassimba
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini