Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amepiga marufuku tabia ya baadhi ya masoko kupangisha vizimba kwa madalali kisha madalali hao kuwapangishia wananchi kwa bei ya juu.
Kunenge amesema jambo hilo linawaumiza wafanyabiashara wadogo wakati lengo la Serikali kujenga masoko hayo, ilikuwa ni kuwasaidia wafanyabiashara na sio kuwakandamiza.
Aidha RC Kunenge amesema masoko yanayojengwa yakikamilika na wafanyabiashara wakapangiwa sehemu za kuuza, bidhaa zao ni marufuku kwa mfanyabiashara kufanya biashara nje ya masoko au sehemu zisizo rasmi.
Akiwa kwenye mradi wa soko la Tandale amemtaka mkandarasi kukamilisha mradi ifikapo mwezi wa nne mwakani, kutokana na umuhimu mkubwa wa soko hilo huku akimtaka mkandarasi wa kampuni ya MECCO inayojenga soko la Kibada kwa gharama za shilingi bilioni 6.6 naye kuhakikisha anakamilisha kabla ya mwezi wa tano mwakani ili wananchi waweze kunufaika na Manispaa ipate mapato.
Social Plugin