JESHI la Polisi Mkoani Tanga limepiga marufuku madisko toto wakati wa sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya kutokana na kwamba baadhi waendeshaji wake kutokuwa waangalifu na kupelekea kuingiza idadi kubwa watu hatua ambayo inapelekea kukosekana kwa hewa na hivyo kusababisha baadhi ya watoto kukanyagana na hatimaye kupoteza maisha.
Marufuku hiyo ilitolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Blasius Chatanda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna walivyojipanga kuimarisha ulinzi kwenye sikukuu za krismas na mwaka mpya ambapo alisema wameamua kupiga marufuku hiyo ili kuepukana na matukio ya namna hiyo ambayo yamekuwa yakijitokeza maeneo mbalimbali hususani wakati wa sikukuu kama hizo.
Kamanda Chatanda alisema wameamua kufanya hivyo kutokana na tabia ya baadhi ya wanaofanya shughuli hizo kutokuwa waangalifu kwenye na idadi ya watoto wanaoingia matokeo yake wanaiingia wanaozidi kupita kiasi hali ambayo inasababisha msongamano mkubwa na kupelekea watoto kukanyagana ikiwemo kukosa hewa na kusababisha madhara kwao.
“Tumepiga marufuku aina yoyote ya madisko toto katika kipindi cha sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kutokana na baadhi ya waendeshaji wake kutokuwa waangalifu na kupelekea kuingiza idadi kubwa ya watu na kusababisha kukosekana kwa hewa na kusababisha kukanyagana na wakati mwengine kupoteza maisha”,alisema.
“Lakini pia nishauri wenye maeneo ya kumbi za stahere wawe na tahadhari ya ulinzi wa ndani kwa sababu hawawez kujua walioingia wana nia gani hivyo wahakikishe wanakuwa makini kwa lengo la kuepusha kutokea matukio ambayo yanasababisha uvunjifu wa amani kwenye maeneo yao “,alisema.
Aidha alisema Jeshi hilo limejipanga vizuri kwa kufanya doria za kutosha barabarani ikiwemo magarai ya kuzunguka kila kona,ulinzi katika maeneo ya idaba na kumbi za sherehe ikiwemo kwenye maeneo ya bahari kuhakikisha watu hawatumii fursa hiyo kuja Tanga kufanya uhalifu kupitia sehemu hizo.
“Lakini tunawaomba watu wa Tanga wafanyae yafuatayo wakati wa sikukuu hizo wasiendeshe vyombo vya moto wakiwa wamelewa kipindi cha sikukuu kwani kuna misingamano mikubwa ya watu watatoka kwenda kutembele na watoto wanakwenda ukijikuta hivyo ni boda wasiendesha iuli kuokoa maisha ya watumiaji wa barabara”,alisema RPC Chatanda.
Hata hivyo aliwataka wananchi ambao wanatoka majumbani mwao wasiache nyumba wazi badala yake wawepo watu ambao wanaweza kulinda nyumba kwani unaweza kuibiwa hata na mpangaji mwenzako bila kujua hivyo ni muhimu uwepo ulinzi.
“Lakini niwaambie kwamba wanaodhani kipindi hiki cha sikukuu wanaweza kufanya lolote watafute kazi nyengine ya kufanya kwa maana sisi kama Jeshi la Polisi hatutakubali kuona watu wachache wanaharibu usalama wa wananchi na watashughulikiwa ipasavyo”,alisema.
Hata hivyo Kamanda huyo aliwatoa hofu wakazi wa mkoa huo kwamba watasheherekea sikuuu kwa amani na utulivu kutokana na kwamba wao wamejipanga vizuri kuhakikisha maeneo yote ikiwemo makanisani na kumbe za burudani ikiwemo fukwe za baharu kuna kuwa na usalama wa kutosha hivyo wasiwe na mashaka.
“Niseme tumejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Tanga wanasheherekea sikuuu hizo kwa amanai na utilivu kuhakikisha hakuna kinachotokea, kwa sababu tuna vitendea kazi vya katika maeneo ya nchi kavu mpaka majini”,alisema RPC Chatanda.
Social Plugin