Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi akisoma majina ya Mawaziri pamoja na Manaibu Mawaziri walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Desemba, 2020 Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. PICHA NA IKULU
. Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumamosi Desemba 5, 2020 amefanya uteuzi wa mawaziri 21 na naibu mawaziri 23 huku akiwateua waliokuwa makatibu wakuu wa wizara kuwa wabunge na kisha kuwateua kuwa mawaziri.
Pia kiongozi mkuu huyo wa nchi ameanzisha wizara mpya ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na kumteua mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile kuwa waziri wa wizara hiyo na Kundo Mathew kuwa naibu waziri.
Akitangaza uteuzi huo katibu mkuu kiongozi, Balozi John Kijazi amesema uteuzi wa mawaziri wawili, Profesa Palamagamba Kabudi (Mambo ya Nje) na Dk Philip Mpango (Fedha) unaendelea na hivyo kufanya idadi ya mawaziri kuwa 23 na naibu mawaziri 23.
Walioteuliwa kuwa wabunge na kisha uwaziri ni Dk Dorothy Gwajima aliyekuwa naibu katibu mkuu Tamisemi akishughulikia sekta ya afya pamoja na Dk Leonard Chamuriho ambaye alikuwa katibu mkuu Wizara ya Uchukuzi.
Majina ya walioteuliwa
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa- Elias Kwandikwa
Utumishi na Utawala Bora- Kapten John Mkuchika
Wizara ya Ardhi- William Lukuvi
Wizara ya Maji- Juma Aweso
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Innocent Bashungwa
Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu- Jenista Mhagama
Wizara ya Afya- Dk Dorothy Gwajima
Ofisi ya Rais Uwekezaji- Profesa Kitila Mkumbo
Wizara ya Katiba na Sheria – Dk Mwigulu Nchemba
Wizara ya Elimu- Profesa Joyce Ndalichako
Wizara ya Mifugo na Uvuvi- Mashimba Ndaki
Wizara ya Maliasili na Utalii- Dk Damas Ndumbaro
Tamisemi- Suleiman Jafo
Wizara ya Nishati- Dk Medard Kalemani
Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi- Dk Leonard Chamuriho
Wizara ya Kilimo- Profesa Adolf Mkenda
Wizara ya Madini- Doto Biteko
Wizara ya Viwanda na Biashara- Godfrey Mwambe
Wizara ya Mambo ya Ndani- George Simbachawene
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Ummy Mwalimu
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Dk Faustine Ndugulile
Naibu mawaziri
Wizara ya Viwanda na Biashara- Kigae Silaoneka
Wizara wa Ardhi- Angelina Mabula
Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira- Patrobas Katambi
Wizara ya Mambo ya Ndani- Hamis Hamza Hamisi
Wizara ya Fedha- Mwanaida Ali Khamis
Wizara ya Elimu- Kipanga Juma Omar
Tamisemi- Dk Festo Ndugange
Wizara ya Nishati- Stephen Byabato
Menejimenti Utumishi wa Umma- John Ndejembi
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari- Kundo Mathew
Wizara ya Mifugo- Pauline Gekul
Wizara ya Madini- Ndulane Kumba
Wizara ya Ujenzi- Godfrey Kasekenya
Ofisi ya Waziri Mkuu wenye ulemavu- Ummy Ndelinanga
Wizara ya Maji- Maryprisca Mahundi
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo- Abdallah Ulega
Ofisi ya Makamu wa Rais (muungano na mazingira)- Mwita Waitara
Wizara ya Mambo ya Nje- William Olenasha
Wizara ya Maliasili na Utalii- Mary Masanja
Ofisi ya rais Tamisemi- David Silinde
Wizara ya Kilimo- Hussein Bashe
Wizara ya Afya- Dk Godwin Mollel
Wizara ya Katiba na Sheria- Pinda Mizengo