Wakati taasisi mbili nchini Marekani Bunge la Seneti na Baraza la Wawakilishi, zilipiga kura kuunga mkono sheria inayoagiza kutolewa fedha kusaidia familia za Wamarekani na makampuni yaliyoathiriwa na Corona, Donald Trump ameamua kutosaini mswada huo.
Mpango huo ulipigiwa kura kwa wingi katika taasisi zote mbili. Maseneta saba tu ndio walipinga. Mpango huu wa msaada ungewezesha familia nyingi kupokea hundi ya dola 600 mapema wiki ijayo, kama alivyoahidi Waziri wa Fedha Steven Mnuchin.
Donald Trump anataka sheria iliyorekebishwa ambayo itamuwezesha kila mtu mzima apokee dola 2,000 kuliko dola 600.
Sheria, iliyokataliwa na rais Donald Trump, ilikuwa inatoa dola bilioni 900 kusaidia familia na wafanyabiashara walio katika matattizo na dola bilioni 1.4 kufadhili matumizi ya serikali.
Kushindwa kuidhinishwa kwa sheria hii ya fedha kunaweza kuwa na athari mbaya: bila saini ya rais, serikali ya Marekani inaweza kusitisha shughuli zake Jumatatu ijayo, Desemba 28.
Social Plugin