RAIS TSHISEKEDI WA DRC AVUNJA MUUNGANO NA KABILA


 Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amevunja muungano ambao umekuwa ukitawala nchi hiyo kwa miezi 16.

Katika hotuba yake kwa taifa, Tshisekedi amesema muungano baina  ya  chama chake cha CACH na chama cha FCC cha rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila hauko tena.

Katika hotuba iliyoandikwa kwa lugha ya Kifaransa na lugha nyingine nne za kitaifa, Rais Tshisekedi, amesema walio wengi nchini DRC wameutaja muungano wa CACH-FCC kuwa chanzo cha matatizo ya sasa ya kisiasa nchin humo.

Tshisekedi amesema serikali yake inalenga kutekeleza mabadiliko katika sekta za uchumi, siasa na usalama na pia katika jeshi na sheria za uchaguzi.

Jitihada za kuwapatanisha Tshisekedi na Kabila zimefeli hata baada ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kujaribu kumshawishi Tshisekedi alegeze msimamo.

Changamoto aliyonayo sasa Rais Tshisekedi ni ya waziri mkuu  Sylvestre Ilunga  ambaye ni kutoka chama cha FCC.

Kwa mujibu wa katiba ya DRC, rais hawezi kumfuta kazi waziri mkuu na sasa anasubiri kuona iwapo atajiuzulu.

Muungano wa FCC unautuhumu ule wa CACH unaoongozwa na Rais Thsisekedi kuwa na mpango wa kuwahonga wabunge wa muungano wa FCC ili kumaliza nguvu yake katika Bunge la Kitaifa ili kulidhibiti. Tshisekedi ametoa tishio kuwa atalivunja bunge iwapo hatapata wingi wa viti unaohitajika.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post