Rais wa zamani wa Ufaransa, Valéry Giscard d'Estaing, kati ya mwaka 1974 hadi 1984, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94.
Kwa mujibu wa familia yake, Giscard d'Estaing, alifariki kutokana na changamoto wa kupumua zilizosababishwa na maambukizi ya Covid 19.
Mwanasiasa huyu aliyekuwa na msimamo wa katim aliyeunga mkono umoja wa Ulaya na pia kupitisha sheria kuhusu masuala ya kuachana katika ndoa, kuruhusu utoaji mimba na matumizi ya dawa za uzazi wa mpango, ni miongoni mwa masuala yaliyompa umaarufu wakati wa utawala wake wa miaka 7.
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema utawala wake uliibadilisha Ufaransa na bado sera zake nyingi zimeendelea kusaidia mabadiliko.
“Alikuwa mtumishi wa uma, mwanasiasa wa maendeleo na uhuru, kifo chake kimeitumbukiza Ufaransa katika majonzi,” ilisema taarifa ya rais Macron.
Familia yake tayari imesema Valéry Giscard d'Estaing, atazikwa kwa kuzingatia masharti ya kiafya na katika shughuli itakayofanyika kwa usiri.