Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS WA ZANZIBAR DR MWINYI AUNDA TUME YA UCHUNGUZI, KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO LA KIHISTORIA LA BAIT-AL JAIB


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi ameunda Tume ya uchunguzi, kufuatia kuanguka kwa jengo la kihistoria la Bait-Al Jaib lililoko eneo la Mji mkongwe Visiwani Zanzibar.

Dkt. Mwinyi ametangaza kuunda Tume hiyo wakati wa mkutano wake na Wadau wa Mji Mkongwe, mkutano uliokuwa na lengo la kuweka mikakati yenye lengo la kuhakikisha matukio kama hiyo hayatokei tena.

Amesema baadhi ya Wajumbe watatoka miongoni mwa Wadau hao wa Mji Mkongwe.

Wakati wa mkutano huo Dkt Mwinyi amewashukuru watu wote waliofanya jitihada kubwa kuhakikisha wanawaokoa na kuwahudumia watu waliokuwamo ndani ya jengo hilo wakati linaanguka.

Jengo hilo linalojulikana sana kama nyumba ya maajabu, lilianguka wakati likiendelea kufanyiwa ukarabati.

Jengo hilo la kihistoria la Bait-Al Jaib ni miongoni mwa majengo ya urithi wa dunia yanayotambuliwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO).


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com