Waziri
wa Viwanda na biashara Mhe. Geoffrey Mwambe akizungumza wakati kufungua
mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya viwanda vidogo
na biashara ndogo hapa nchini uliofanyika Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Profesa Riziki Mdoe
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera
ya maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini
uliofanyika Jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe wa tatu kutoka
kushoto waliokaa msitari wa mbele akiwa katika picha ya pamoja na
wajumbe wa mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya maendeleo ya
viwanda vidogo na biashara ndogo hapa nchini mara baada ya ufunguzi wa
mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma.
Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Serikali imesema imejipanga kuboresha elimu ya
ujasiliamali kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuanzisha biashara
ikiwa ni njia mojawapo ya kuwainua wananchi kuwa na wafanyabiashara na
wawekezaji wengi hapa nchini.
Hayo yamebainishwa Jijini Dodoma na Waziri wa Viwanda
na Biashara Mhe. Geoffrey Mwambe, akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kufungua mkutano wa wadau kuhusu rasimu ya sera ya
maendeleo ya viwanda vidogo na biashara ndogo ambapo amesema kuwa moja
ya vikwanzo vinavyosababisha watanzania kushindwa kupiga hatua kwenye
biashara ni ukosefu wa elimu ya ujasiriamali.
Ameongeza kuwa pamoja na matatizo ya ukosefu wa
masoko ya bidhaa mbalimbali na mitaji lakini elimu bado ni kikwazo
kikukwa kwa watanzania katika kuanzisha biashara zao wenyewe.
“Watanzania bado hii elimu ya ujasilimali ni sulaa
geni kidogo kwetu leo hii mtanzania anakwenda chuo cha biashara kusoma
ili aje kuwa msimamizi wa biashara ya mtu na siyo kubuni yake ”amesema
Mhe. Mwambe
Amebainisha kuwa kutokana na hali hiyo alivitaka vyuo
vya elimu ya biashara nchini pamoja na taasisi mbalimbali kuweka
utaratibu wa kutoa mafunzo ya ngazi mbalimbali ili kuwajenga uwezo watu
kwenda kuanzisha biashara zao.
“Leo hii unakuta chuo cha elimu ya biasahra kama CBE,
kinafundisha mtu kwenda kuwa msimamizi wa biashara ya kampuni furani
lakini yeye mwenyewe siyo mfanyabiashara inabidi tubadilike hivi
karibuni nilikuta na na Mo Dewji akanambia anasoma masters ya biashara
Dubai hata sisi wajasiriamali wadogo lazima tusome ili kuwa
wafanyabiashara na siyo wasimamizi” amesema.
Kuhusu rasimu hiyo ya sera ya maendeleo ya viwanda
vidogo na biashara ndogo, amewata wajumbe wa mkutano huo kufanya
maboresho ili ipatikane sera itakayo saidia sekta hiyo kukua zaidi hapa
nchini.
“Lazima mtoke na maboresho ya sera ambayo itakwenda
kutambua viwanda vidogo pamoja na biashara ndogo kwani ndizo ambazo
zimewatoa watu wengi hapa nchini” amesema.
Aidha amefafanua kuwa
serikali imekuja na rasimu ya sera hiyo kutokana iliyokuwepo awali kuwa
ya muda mrefu na haikidhi mahitaji ya sasa katika ulimwengu wa Sayansi
na Taknolojia.
“Lakini changamoto
nyingine katika sera ile ya awali ni ilijengwa katika malengo ya sekta
moja tu ya viwanda ndiyo maana akawa zaidi chini ya SIDO, lakini hivi
sasa biashara ndogo zipo katika sekta nyingine pia kama vile mahoteli”
amesema.
Pia amesema sera hiyo mpya itakuwa na uwezo wa
kuwawezesha wajasiriamali wadogo kukuwa kutoka ngazi ya chini na kuwa
wafanyabiasahra wakubwa hali itakayo saidia kuongeza walipa kodi na
taifa kupata mapato.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin