SERIKALI YAWATAKA WALIOHUJUMU MALI ZA VYAMA VYA USHIRIKA KUZIREJESHA MARA MOJA

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akizungumza wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira,akiongea kwenye kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mrajis wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege,akiwasisitiza jambo washiriki wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Bodi ya KCBL, Dk Gervas Machimu,akizungumza wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Kilimanjaro Co-operative Bank Limited (KCBL), Balozi Ibrahim,akitoa maelezo kwa washiriki wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma.

Afisa Mkuu wa biashara wa CRDB, Dk. Joseph Witts,akizungumza wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma

Baadhi ya washiriki wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya,akiteta jambo na Mrajis wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL) lililofanyika jijini Dodoma


Na.Alex Sonna,Dodoma.

SERIKALI imewataka watu wote waliohujumu mali za vyama vya ushirika kujisalimisha na kurudisha mali hizo kwa hiari kabla ya kuchukuliwa hatua za Kisheria.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Kusaya wakati wa kongamano la uwekezaji na ununuzi wa hisa na amana za benki ya Ushirika ya Kilimanjaro (Kilimanjaro Cooperative Bank Limited (KCBL).

Kusaya amesema kuwa mali zote za vyama vya ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu zitarudi kwenye mikono ya serikali.

Aidha,amebainisha kuwa wamefanikiwa kurejesha mikononi mwa serikali mali 59 za ushirika zilizochukuliwa bila kufuata utaratibu kuna viwanja,, majumba, mitambo na vingine vyote vina thamani ya bilioni 68.9 na zoezi ni endelevu.

“Kama kuna mtu ana mali za ushirika kwa njia zisizo sahihi azirudishe kwa hiari bila hivyo tuna nguvu nyingi za ziada haijalishi zipo wapi lazima tutazipata,” amesema Kusaya.

Kusaya ameendelea kubainisha kuwq serikali itakuwa bega kwa bega na benki hiyo ua ushirika ya Kilimanjaro ili kuhakikisha inazaa matunda kwa manufaa ya Watanzania.

“Kama tunaamini katika ushirika lazima tuuheshimu na kulenga kufanya ushirika wa kibiashara katika kumkomboa Mtanzania tunataka kila mwanaushirika awe bilionea,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa bodi ya KCBL, Dk Gervas Machimu amesema benki hiyo iko imara kwa ajili ya kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt.Machimu amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya CRDB na wana bodi ya pamoja kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.

Hata hivyo ameelezea kuwa Serikali inayo ndoto ya kuendeleza viwanda katika nchi na kutoa huduma katika kilimo na biashara na uwepo wa benki hiyo utasaidia kuendeleza sekta za uzalishaji na kusaidia zaidi ya asilimia 60 ya Watanzania wanaotegemea kilimo kunufaika.

Naye Mrajis wa vyama vya ushirika Dk Benson Ndiege amesema kuwa KCLB ni chama cha ushirika kilichoandikishwa kama benki na kimepata leseni ya kuhudumu kama benki ya ushirika kwa wananchi wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Tanga katika kilimo cha kahawa.

Amebainisha kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo, ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro na benki ya CRDB wamefanya kila liwezekanalo ili benki isimame na kuhudumia makundi mbalimbali kama wakulima, wafugaji, wavuvi, wajasiriamali, wafugaji.

“Kama tukiamua leo kuikuza benki hii kwa kununua hisa tunaweza kuifikisha mbali, vyama vikuu vya ushirika viko 46 lakini vinavyofanya kazi vizuri viko 30,” amesema

Amesema benki ya ushirika ya Kenya inafanya vizuri kutokana na uwezezaji uliofanyika na Tanzania ikiamua jambo hilo hakuna linaloshindikana.

“Kama tukifanya mabadiliko kwenye sekta ya kilimo, viwanda na uvuvi kama walivyofanya Kenya na kwenye benki ya ushirika wana uwekezaji ndio maana wamefanikiwa na benki yao ni ya tatu kwa ukubwa Kenya,” amesisitiza Dk.Ndiege

Mwenyekiti wa Kilimanjaro Co-operative Bank Limited (KCBL), Balozi Ibrahim amevitaka vyama vya ushirika kuchangamkia fursa ya uwekezaji kwenye vyama hivyo.

Amesema wanachama wengi wa KDF wamewekeza kwenye benki hiyo.

Ofisa Mkuu wa biashara wa CRDB, Dk. Joseph Witts amesema kuwa CRDB iliundwa na ushirika na baadaye kuwa benki ya biashara.

Amesema wana kitengo cha kutoa mikopo kwa wakulima na wazalishaji mbalimbali.

“Mikopo yote tunayoitoa kwenye kwenye vyama vya ushirika inalipwa vizuri,” alisema

Amebainisha wametoa bilioni saba kama mtaji kwenye benki ya KCBL.

Amesema CRDB ina menejimenti ndani ya benki hiyo na wajumbe wa bodi ya CRDB wengine wako kwenye benki ya KCBL ili kuweza kuborsha utendaji

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post