Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) akisisitiza jambo wakati akitoa elimu ye Lishe bora kwa madiwani wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma |
Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) akisisitiza jambo wakati akitoa elimu ya Lishe bora kwa madiwani wa Halmashauri ya Kongwa mkoani Dodoma |
MKUU wa wilaya ya Kongwa kulia Dkt Selemani Serera kulia akiwa na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) wa tatu kushoto wakifuatilia kwa umakini michango ya madiwani wakati wa semina ya lishe bora
katikati ni Mkurugenzi Halmashauri wa Kongwa Dkt Omary NkulloMKUU wa wilaya ya Kongwa kulia Dkt Selemani Serera kulia akiteta jambo na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) wa pili kushoto wakati wa semina ya lishe bora katikati ni Mkurugenzi Halmashauri wa Kongwa Dkt Omary Nkullo
Sehemu ya madiwani wakifuatilia matukio mbalimbali
MADIWANI wa Halmashauri ya Kongwa wilayani Kongwa Mkoani
Dodoma wamekuwa viongozi wa kwanza wa kisiasa hapa nchini kupatiwa
elimu ya lishe bora.
Mnamo
2019, Shirika la Agri Thamani Foundation lilianzisha na kuratibu
mchakato wa ajenda ya Lishe Bora kuwa kipaumbele na kuingizwa kwenye
Ilani za Uchaguzi 2020-2025 za Vyama vya Siasa 3 nchini; Chadema, ACT
Wazalendo na Chama Tawala - Chama Cha Mapinduzi.
Baada
ya kufanikiwa kuingiza Ajenda ya Lishe katika Ilani za Uchaguzi
2020-2025 za Vyama vyote 3 huku Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ilienda
mbali zaidi kwa kuanisha kwa kina malengo yake katika kuimarisha hali ya
Lishe nchini, Agri Thamani imeanzisha programu ya kutoa mafunzo ya
lishe bora kwa Madiwani.
Programu
hii imezinduliwa kwa kutoa mafunzo ya lishe bora kwa mara ya kwanza
wilayani Kongwa kwa lengo la kuwapa Madiwani uelewa mpana wa ajenda hii
na kuwawezesha kusimamia utekelezaji wake.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wa mpango huo wa Elimu ya Lishe Bora; Mkurugenzi wa
Taasisi hiyo Neema Lugangira (MB) alisema wameamua kutoa elimu hiyo ili
ikawe chachu kwa jamii kubadiliana na kuondokana na tatizo la lishe
kwenye maeneo yao.
Alisema
kutokana na kwamba madiwani hao wanaongoza idadi kubwa ya wananchi huku
wakiwa na ushawishi mkubwa kwa jamii wanayoiongoza hivyo elimu ya lishe
bora itasaidia jamii kuweza kutambua na kuepukana na suala la lishe
duni.
Kwa kuanzia Elimu ya Lishe Bora itatolewa kwa Madiwani kwa makundi kutoka Mkoa wa Dodoma, Tabora, Kigoma, Tanga na Kagera.
Awali
akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Dkt Selemani
Serela aliishukuru Taasisi hiyo kwa kuona umuhimu kwa kutoa elimu kwa
madiwani hao na kueleza itakuwa ni chachu ya elimu hiyo kuendelezwa
zaidi.
Alisema kwamba
wanaomba pia ushirikiano wa elimu ambayo imeitolewa inahitajika iendele
zaidi huku akitaka lazima wachukue hatua kwa vitendo ili kuondokana na
suala la lishe duni kwenye jamii.
“Lazima
tuchukue hatua kwa vitendo, tunategemea tuone namna gani tunaweza
kufikia hatua ambazo tumekubaliana hapa na tuwe na mpango kazi
unaopimika ”Alisema
Aidha
alisema pia leo ilikuwa ni hatua ya kwanza ya kuwasilisha mada hivyo
wanategemea kuona mikakati inawekwa ya namna gani wanaweza kufikia hatua
ambazo wamekubaliana.
“Tutakaa
kama wilaya tuone tunafanyaje madiwani wanafanya kazi kubwa sana
tunahitaji wataalamu mnapokuja kila mara kutuongezea uelewa hatua ambayo
itasaidia kuibadilisha jamii. Tunahitaji pia Agri Thamani muungane nasi
katika jitihada hizi hapa Kongwa “Alisema DC huyo
Naye
kwa upande wake Afisa Lishe wa wilaya ya Kongwa Maria Haule alisema
wamekuwa wakifanya shughuli wakilenga makundi yaliyopo kwenye hatari
kubwa ya kupata changamoto ya lishe duni hasa matunzo yasipokuwa vizuri.
Alisema
takwimu zinaonyesha mkoani Dodoma asilimia 37.2 ya watoto chini ya umri
wa miaka 5 wana udumavu. Takwimu hizi ni kwa mujibu wa TNNS 2018.
Maria
alisema lakini pia takwimu halmashauri za afya zinaonyesha asilimia 24
ya upungufu wa damu na asilimia 0.1 ya ukondefu kwa watoto chini ya
miaka mitano.
Alisema wao kama wilaya wana mikakati kukabiliana na hiyo changamoto ikiwemo kutenga fedha kwa ajili ya afua za lishe.
Alieleza
huku akitolea mfano kwa mwaka huu wa fedha wametenga milioni 77.5
ambapo hiyo ni kwa mujibu wa Sera ya Serikali kila mtoto aliyechini ya
umri wa miaka 5 anatengewa sh 1,000 kwa ajili ya afua za lishe.
Afisa
Lishe huyo alisema katika hiyo bajeti ipo inayosaidia kugharamikia
matibabu kwa watoto wenye utapiamlo mkali na pia wametenga milioni 32
kwa ajili ya chakula la dawa na vifaa tiba ikiwemo kuwajengea uwezo
watoa huduma za afya vituo namna ya kuendelea kuelimisha jamii kwenye
masuala la lishe na kutibu wenye watakaonekana wana lishe duni.
Afisa
Lishe alisisitiza umuhimu wa Agri Thamani kuwa na ofisi Kongwa ili
waweze kushirikiana kwa karibu katika kutokomeza changamoto ya udumavu
na utapiamlo kwa ujumla wilayani Kongwa.
Hata
hivyo Diwani wa Viti Maalumu (CCM) anayetokea wilaya ya Kongwa Fatuma
Diria aliishukuru Agri ThamanI kwa kutoa semina hiyo na kwa kweli
wamejifunza mambo mengi mazuri na yenye manufaa kwao na kwa jamii.
Alisema
wakati mwengine nilikuwa naelewa lakini nilikwa naona kuna watoto
wanasoma shule hawana uwela sikujua kwamba chanzo kinaanzia kwa mama
mjamzito kutokana na lishe duni wakati mama akiwa mjamzito .
Hata
hivyo alisema kwa kupata elimu hiyo atakwenda kuwa balozi wa
kuihamasisha jamii kuhakikisha inachukua hatua za kukabiliana na tatizo
hilo kwa kupata lishe bora.
Kwa
upande wake, Mkurugezi wa Halmashauri ya Kongwa ameishukuru sana Agri
Thamani kwa kuanzia Kongwa na ameahidi Kongwa itakuwa Halmashauri ya
Mfano kwenye Lishe. Alimalizia kwa kuikaribisha sana Agri Thamani Kongwa
ili wafanye kazi pamoja.