TBS YAENDELEA KUTOA ELIMU YA VIWANGO KATIKA MAONESHO YA TANO YA BIDHAA ZA VIWANDANI

Waziri mteule wa Viwanda na Biashara Mhe. Geofrey Mwambe (Mb) akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Uhusiano wa TBS Bi.Neema Mtemvu pindi alipotembelea Maonesho ya Viwanda yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.


Shirika la Viwango Tanzania (TBS)limeendelea kutoa huduma zake katika Maonesho ya Bidhaa za Viwanda yanayofanyika katika Viwanja Maonesho vya Mwl. Nyerere (Sabasaba) Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho hayo yanayofanyika kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam jana maarufu kama Saba Saba, Afisa Uhusiano wa TBS, Neema Mtemvu alisema maonesho hayo pia yamekuwa fursa muhimu ya wao kusikiliza maoni ya wadau hao.

"Ushiriki katika haya maonesho umetufanya tuweze kukutana na wadau wenye viwanda,wananchi, wajasiriamali na kuweza kuwaelimisha kuhusu masuala ya viwango pamoja na kusikiliza changamoto zao". Amesema Bi.Neema.

Aidha Bi.Neema amesema watu ambao walikuwa wanatarajia kuwapata wamefanikiwa kuwapata kwani muitiko umekuwa mkubwa na maonesho yanaenda vizuri.

Amesema wazalishaji wakipata alama ya ubora wanaweza kufikia masoko mbalimbali hasa ya Afrika Mashariki na zitaweza kuvuka mipaka ya nchi hizo bila vikwazo vyovyote.

Pamoja na hayo Bi.Neema amesema TBS inawahimiza wahakikishe wanazalisha bidhaa zilizo na ubora hatua itakayosaidia kulinda mitaji yao na kuhimili ushindani kwenye soko.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post